HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 27 February 2019

VIGOGO WATATU WA RAHCO KUSOMEWA MAELEZO YA AWALI MWEZI UJAO

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga kuwasomea maelezo ya awali (PH), Machi 3, 2019 vigogo watatu wa kampuni Hodhi ya mali za Reli, (Rahaco).

Hatua hiyo imefikwa leo Februari 27.2019 baada ya upande wa mashtaka mara ya mwisho kuitaarifu mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo umeishakamilika na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuipatia mamlaka mahakama hiyo ya Kisutu kusikiliza kesi hiyo.

katika kesi hiyo, watuhumiwa wanakailiwa na mashtaka nane ya uhujumu uchumi likiwemo shtaka la kuisababishia Serikali hasara ya USD 527,540.

Mapema wakili wa Serikali, Maghela Ndimbo alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba, alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilka hivyo aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya usikilizwaji wa awali. hata hivyo, kabla ya kesi hiyo kuahirishwa washtakiwa walisomea upya mashtaka yao ambapo wote kwa pamoja walikana kutenda makosa hayo.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Rahco, Benhardard Tito, Mwanasheria wa zamani wa kampuni hiyo, Emmanuel Massawe na mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wadaiwa kati ya Septemba Mosi, 2014 na Septemba 30, 2015 kwa nia ya kutenda kosa walikula njama kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Tito, anadaiwa kuwa Februari 27, 2015 katika ofisi za Rahco zilizopo Ilala alitumia madaraka yake vibaya kwa kuiajiri Kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Ltd kama mshauri wa mradi wa uimarishaji wa reli ya kati, bila idhini ya Bodi ya Rahco.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad