HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 11, 2019

TUNAMFUNGA AL AHLY KATIKA UWANJA WETU WA NYUMBANI - SIMBA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MTANANGE wa michuano ya Klabu Bingwa kati ya timu ya Simba na Al Ahly y Nchini Misri unatarajiwa kuchezwa kesho katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo umebakiza masaa machache kuweza kufikia majira ya saa 10 alasiri ya Februari 12, 2019.

Kuelekea mechi hiyo, Nahodha wa timu ya Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesema kuwa anaamini mchezo huo utakuwa ni mgumu kwao ila watahakikisha wanautumia vizuri uwanja wa nyumbani. Tshabalala amesema, katika mchezo wa kwanza walipoteza kwa goli nyingi sana ila alama zinazopatikana ni tatu kwahiyo wao kama wachezaji wamejizatiti kuweza kupata alama hizo wakiwa nyumbani.

“Tunaamini mchezo wetu wa kesho tunashinda na kikubwa ushindi wowote tutakaoupata alama ni zile zile tatu, ingawa wao walitufunga kwa goli nyingi ila sisi tutatumia uwanja wetu wa nyumbani kupata matokeo,”amesema. Amesema, kikubwa ni wachezaji kujituna uwanjani katika dakika zote 90 na pia mashabiki kujitokeza kwao kwa wingi uwanjani ni moja ya hamasa kubwa sana kwao. 

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa klabu ya Al Ahly kutoka Uarabuni amesema haiofii klabu ya Simba kwani waliweza kupata matokeo wakiwa nyumbani kwa ushindi mnono wa goli tano na wanaamini wanaweza kushinda tena hata wakiwa ugenini.

Simba atashuka tena dimbani  na Waarabu mapema kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar, ambapo katika kundi D Al Ahly amekuwa kinara kwa kuwa na alama 7 akifuatiwa na Alh Alhy mwenye alama 4, Simba akishika nafasi ya tatu kwa alama 3 na JS Saoura akiwa na alama 2. Ikumbukwe  katika mchezo wao kwa kwanza uliopigwa Februari 02 dhidi ya Al Alhly Simba alikubali kupigo cha goli 5-0 akiwa ugenini nchini Misri.
Nahodha wa Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuelekea mchezo wao wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Alh Alhly utakaochezwa kesho katika dimba la Uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad