HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 12 February 2019

Serikali yaunga mkono juhudi za Dk Mengi kuanzisha maabara ya kisasa ya kutumia tiba ya seli shina

Serikali imesema inaunga mkono jitihada za Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi za kuanzisha nchini maabara ya kisasa ya kutumia tiba ya seli shina (Stem Cell), kwa madhumuni ya kutibu magonjwa  mbalimbali  yasiyo na tiba hadi sasa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akifungua kongamano la Kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya seli shina ( stem cells) kwa magonjwa  ambayo hadi sasa hayana tiba.
Amesema licha ya kuwa Tanzania imeiboresha sana sekta ya afya kuna umuhimu jitihada hizo za serikali kuungwa mkono na wadau wa sekta binafsi.
Mapema akimkaribisha mgeni rasmi kufungua kongamano hilo Mwenyekiti Mtendaji wa IPP limited Dr Reginald Mengi amesema kusudio lake la kuanzisha maabara hiyo ya utafiti wa kisasa ni kutoa mchango wake katika kuiwezesha Tanzania kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa ya binaadamu ambayo hayana tiba kwa sasa.
Aidha Mratibu Mipango wa Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation iliyoandaa kongamano hilo, Dr. Michael Magotti, na mwenzie  Dr Kampon Sriwatanakul wamesema wanakusudia kuleta wazo jipya kuhusu  tiba nchini na kwamba wameshapeleka maombi serikalini ya kuomba vibali vya kuanzisha maabara hiyo na lengo la kongamano hilo ni kuongeza uelewa kuhusu aina hiyo mpya ya matibabu kutoka kwa madaktari wabobezi kutoka nchi mbalimbali duniani.
Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya afya na tiba, huku kukiwa na mamilioni ya watu wenye ulemavu mbalimbali barani Afrika wakibaki majumbani kwao kwa kukosa uwezo wa kupelekwa India au nchi nyingine zilizoendelea ili kupatiwa matibabu.
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP limited Dr Reginald Mengi (kulia) akiongozana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile (kushoto) kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kufungua kongamano la Kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya kutumia seli shina (Stem Cell) kwa magonjwa ambayo hayana tiba, lililofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni mstari wa nyuma kutoka kushoto ni Mkuu wa Ubora wa Huduma Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dr. Tulizo Sanga, Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia pamoja na Mratibu Mipango wa Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation iliyoandaa kongamano hilo, Dr. Michael Magotti.
 Mratibu Mipango wa Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation iliyoandaa kongamano hilo, Dr. Michael Magotti akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na washiriki (hawapo pichani) wakati kongamano la Kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya kutumia seli shina (Stem Cell) kwa magonjwa ambayo hayana tiba, lililofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya seli shina (Stem Cell) kwa magonjwa  ambayo hadi sasa hayana tiba lililoandaliwa na Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation na kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP limited Dr Reginald Mengi akizungumza dhumuni lake la kuanzisha maabara ya kisasa ya tiba kwa kutumia seli shina (Stem Cell), kwa madhumuni ya kutibu magonjwa mbalimbali yasiyo na tiba hadi sasa wakati wa kongamano la kwanza la Kimataifa kuhusu tiba hiyo lililoandaliwa na Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation na kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Mishipa ya Fahamu ya Ubongo na Uti wa Mgongo kutoka India, Prof. Alok Sharma (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP limited Dr Reginald Mengi (wa pili kulia) zawadi ya kitabu alichokiandika kuhusu matibabu ya kutumia seli shina (stem cell) kwa magonjwa sugu yanayosababisha matatizo ya ubongo na mishipa ya fahamu (Stem Cell Therapy in Neurological Disorders-4th Edition). Wanaoshuhudia tukio hilo ni kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Stem Cell Afrika, Andelene Thysse, Mratibu Mipango wa Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation iliyoandaa kongamano hilo, Dr. Michael Magotti pamoja na Dr. Kampon Sriwatanakul (kulia) kutoka Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation.
 Dkt. Petcharin Srivatanakul kutoka Thailand akitoa mada kuhusu Uanzishwaji wa maabara ya kutengeneza seli shina/chembechembe hai (Stem Cell) kwa magongwa yasiyo na tiba wakati kongamano la Kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya kutumia kinasaba cha kiinitete (Stem Cell) kwa magonjwa hayo ambayo hayana tiba lililoandaliwa na Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation na kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Dkt. Daniel Maeda kutoka Idara ya Biolojia ya Molekyuli na Bayoteknojia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akiwasilisha mada kuhusu “uwezo na changamoto za seli shina za kiinitete na seli shina shawishi” wakati kongamano la Kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya kutumia seli shina (Stem Cell) kwa magonjwa hayo ambayo hayana tiba lililoandaliwa na Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation na kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP limited Dr Reginald Mengi na ugeni wa wataalamu wa tiba ya kutumia seli shina (Stem Cell) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kongamano la Kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya kutumia seli shina (Stem Cell) kwa magonjwa hayo ambayo hayana tiba lililoandaliwa na Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation na kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Balozi mstaafu Juma Mwapachu akiuliza swali wakati kongamano la Kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya kutumia seli shina (Stem Cell) kwa magonjwa hayo ambayo hayana tiba lililoandaliwa na Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation na kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa sekta ya afya na tiba walioshiriki kongamano la kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya seli shina (Stem Cell) kwa magonjwa ambayo hadi sasa hayana tiba lililoandaliwa na Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation na kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP limited Dr Reginald Mengi (katikati) akibadilishana mawazo na Daktari Bingwa wa masuala ya Ngozi kutoka Medical Tourism Fit jijini Dallas-Marekani, Dr. Benedict Olusola (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Touchmate, Bw. Victor Tesha (kulia) wakati wa kongamano la kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya seli shina (Stem Cell) kwa magonjwa ambayo hadi sasa hayana tiba lililoandaliwa na Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation na kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP limited Dr Reginald Mengi akimsalimia Binti mwenye ulemavu uliotokana na ajali ya gari Wakonta Kapunda ambaye ni mshindi wa wazo la kibiashara la shindano la kujenga hoja asili ya ujasiriamali lililojulikana kama “DREAM TO GREATNESS“ lililoandaliwa wakati wa uzinduzi wa kitabu cha “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” alipomwalika kushiriki kongamano la kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya seli shina (Stem Cell) kwa magonjwa ambayo hadi sasa hayana tiba lililoandaliwa na Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation na kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Dr Mengi ni Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Touchmate, Bw. Victor Tesha.
 Picha ya pamoja ya washiriki wa kongamano la kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya seli shina (Stem Cell) kwa magonjwa ambayo hadi sasa hayana tiba lililoandaliwa na Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation na kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti Mtendaji wa IPP limited Dr Reginald Mengi akimkabidhi Mkurugenzi wa Stem Cell Afrika, Andelene Thysse (kulia) kitabu chake cha “I Can, I Must, I Will-The Spirit of Success” wakati wa kongamano la kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya seli shina (Stem Cell) kwa magonjwa ambayo hadi sasa hayana tiba lililoandaliwa na Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation na kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr Faustine Ndungulile akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP limited Dr Reginald Mengi (katikati) mara baada ya kufungua kongamano la kwanza la Kimataifa kuhusu tiba ya seli shina (Stem Cell) kwa magonjwa ambayo hadi sasa hayana tiba lililoandaliwa na Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation na kufanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa IPP Touchmate, Bw. Victor Tesha, Dr. Kampon Sriwatanakul (wa pili kulia) kutoka Kampuni ya IPP Research, Technology and Innovation pamoja na Mratibu wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia (kulia).
No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad