HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 20 February 2019

TFF YATANGAZA KAMATI YA SAIDIA TAIFA STARS ISHINDE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) limetangaza kamati ya saidia Taifa Stars ishinde yenye majina ya watu 14. Kamati hiyo inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda imetangazwa leo na TFF ikiwa na lengo la kusaidia timu ya Taifa ishinde kwenye mchezo wake wa mwisho mwezi Machi mwaka huu.

Taifa Stars inatarajia kucheza mchezo wake wa mwisho wa kufuzu Fainali za mataifa Afrika (AFCON) nchini Misri dhidi ya Uganda ‘The cranes’. Katika kamati hiyo, Makonda atasaidiwa na wadau wa soka tofauti akiwemo Abdalla Bin Kleb, Salum Abdalla, Faraj Asas, Mohamed Dewji, Farouk Barhoza, Mohamed Nassor na Patrick Kahemele.

Wengine ni Teddy Mapunda, Philimon Ntaihaja, Farid Nahid, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro, Ofisa habari wa Simba Haji Manara na Mhandisi Hersi Said ambaye atakuwa katibu wa Kamati hiyo. Taifa Stars inatakiwa ishinde mchezo wake wa mwisho dhidi ya Uganda ili ifanikiwa kuingia kwenye hatua ya Fainali , 

Timu hiyo ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi hilo, ikifikisha pointi tano baada ya kucheza mechi nne, ikifungwa mbili na sare mbili.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad