HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 20 February 2019

TAFF YATOA OMBI KWA SERIKALI KUISAIDIA TIMU YA TAIFA YA WALEMAVU

SERIKALI imeombwa kusaindia Timu  ya Taifa mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu ili wafanye vizuri katika mashindano ya kombe la mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF), Riziki Lulida ambapo amesema ni vema Serikali ikatoa kutoa kipaumbele katika kuisaida timu hiyo ili iibuke na ushindi katika mashindano hayo ya Afrika Mashariki na Kati.

Amefafanua ni imani yao heshima ya nchi inaweza kutengenezwa kupitia timu yoyote hivyo hakuna sababu ya kuzibagua timu kwa kuangalia maumbile yao."Tunatoa ombi kwa Serikali kuisaidia timu hii ili nayo iweze kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ikiwemo hiyo ya Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

Mwenyekiti huyo TAFF ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum(CUF), amesema atawashirikisha wabunge wenzake hasa wenye ulemavu ili waweze kusaidia timu hiyo ya taifa kwani ikisaidiwa itafanya vema katika michuano mbalimbali.

Kuhusu mashindano ya Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Katibu wa TAFF Moses Mabula amesema yataanza kuanzia Juni 22 mwaka huu na yatashirikisha nchi 11 za Ukanda wa Afrika Mashariki.

Amezitaja baadhi ya nchi ambazo zitashiriki kwenye mashindano hayo ni mwenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Sudan Kusini na Sudan huku akifafanua licha ya auhitaji wa misaada mbalimbali hitaji lao kubwa ni kuona Watanzania wengi wanajitokeza katika viwanja wakati wa mashindano hayo.

"Matarajio yao ni kubakiza kombe la mashindano hayo hapa nyumbani Tanzania.Hii ni mara ya kwanza sisi kushiriki mashindano hayo lakini tunaamini tukiiungwa mkono tutafanya vizuri na kuitangaza nchi kimataifa,"amesema.

Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo Juma Kidevu amesema maandalizi yanaendelea vizuri na kuahidi kuibuka kidedea katika mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika nchini na kwamba changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni uhaba wa vifaa kama fimbo za kutembelea, jezi na mipira hivyo wanaomba wadau kujitokeza kuwasaidia.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya maandalizi ya mshindano ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati yanayotarajiwa kufanyika Juni 22 mwaka  huu hapa nchini Tanzania. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad