HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 20 February 2019

WADAU WAISHAURI SERIKALI KUONGEZA BAJETI KATIKA MASUALA YA MTOTO

 Wadau wameishauri Serikali kuongeza kiwango cha Bajeti katika masuala yahusuyo maendeleo na ustawi wa mtoto ili kuwezesha Mipango mbalimbali kutekelezeka katika kumpatia mtoto haki na ustawi wake.

Hayo yamebainika leo jijini Dodoma katika kikao kilichokutanisha Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika ya C-SEMA na SOS-Children Village Tanzania kujadili jinsi ya kuweka Mikakati madhubuti katika kuwezesha ongezeko la Bajeti katika masuala ya watoto nchini.

Akitoa taarifa ya utafiti huo Mwakilishi wa Shirika la SOS-Children Tanzania Bw. Mpelly Ally amesema kuwa utafiti huo uliofanya katika mwaka wa fedha 2015/16 na 2017/2018 umeonesha kuwa kwa kiasi kikubwa fedha zilizotengwa katika Bajeti ya Wizara husika kwa ajili ya masuala ya watoto hakikutolewa na zilizotolewa zilikuwa kwa asilimia ndogo kabisa kuweza kutekeleza afua mbalimbali za watoto nchini.

Ameongeza kuwa mara baada ya kupata matokeo hayo na kubaini kuwa kuna upungufu wa Bajeti katika masuala ya watoto waliamua kuja mapendekezo kadhaa ikwemo Serikali kuisambaza hiyo taarifa kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuona jinsia watakavyosaidia kuwezesha kuondokana na upungufu huo.

Ameyataja mapendekezo mengine kuwa Wizara kutoa elimu kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ili kuweza kujua umuhimu wa kutenga na kuwezesha utoaji wa fedha kwa ajili ya masuala ya  maendeleo na ustawi wa mtoto nchini.

“Kikubwa tunaishauri Serikali iyafanyie kazi mapendekezo yetu ili tuhakikishe mtoto haachwi nyuma kufika maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030”alisema

Akichangia katika kikao hicho Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amesema kuwa ili kuipa nguvu tafiti hiyo wadau hao wanapaswa kuja na sababu yenye mashiko zaidi ya kwanini kuongezeka kwa Bajeti ya mtoto ili kuisaidia Serikali kupambanua na kuja na mikakati madhubuti.

Naye Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi amewataka wadau hao kuja na orodha ya mahitaji na wapi kunahitajika ongezeko la Bajeti katika masuala ya mtoto nchini ili kuwepo na uelewa wa pamoja wa Serikali na wadau katika kulitekeleza hilo.

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu akiongoza kikao jijini Dodoma kilichokutanisha Menejimenti ya Wizara na wadau kutoka Mshirika ya C-SEMA na SOS-Children VillageTanzania kujadili jinsi ya kuweka Mikakati madhubuti katika kuwezesha ongezeko la Bajeti katika masuala ya watoto nchini.
 Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Mathias Haule(kushoto) akielezea dhumuni la kufanyika kwa tafiti iliyobaini kuwepo kwa upungufu wa Bajeti katika masuala ya watoto nchini katika kikao kilichowakutanisha wadau kutoka Mashirika ya C-SEMA na SOS-Children VillageTanzania na Wizara jijini Dodoma kulia waliokaa ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu.
 Mwakilishi wa Shirika la SOS-Children Village Tanzania Bw. Mpelly Ally akiwasilisha matokeo ya tafiti kwa uongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) kuhusu kuwepo kwa upungufu wa Bajeti katika masuala ya watoto nchini katika kikao kilichowakutanisha wadau kutoka Mashirika ya C-SEMA na SOS-Children VillageTanzania na Wizara jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akichangia hoja katika kikao kilichokutanisha Wizara na Wadau jijini Dodoma kutoka Mashirika ya C-SEMA na SOS-Children Village Tanzania kujadili jinsi ya kuweka Mikakati madhubuti katika kuwezesha ongezeko la Bajeti katika masuala ya watoto nchini.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo yaJinsia Bw. Julius Mbilinyi akifafanua jambo katika kikao kilichokutanisha Wizara na Wadau jijini Dodoma  kutoka Mashirika ya C-SEMA na SOS-Children VillageTanzania kujadili jinsi ya kuweka Mikakati madhubuti katika kuwezesha ongezeko la Bajeti katika masuala ya watoto nchini.
Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) wakifuatilia wasilisho kuhusu utafiti uliofanyika kuhusu kuwepo kwa upungufu wa Bajeti katika masuala ya watoto nchini katika kikao kilichowakutanisha wadau kutoka Mashirika ya C-SEMA na SOS-Children Village Tanzania na Wizara.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad