HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 19 February 2019

RC MAKONDA ATIMIZA AHADI YA KUMPATIA MTAJI WA MILIONI 5 MAMA MZAZI WA MAREHEMU MSANII "GODZILLA".

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo ametimiza ahadi aliyotoa ya kumpatia Mama Mzazi wa Marehemu Msanii Godzilla kiasi cha shilingi milioni 5 kama mtaji wa kufungua duka la kisasa la kuuza dawa za binadamu (pharmacy) itakayowezesha familia kujikwamua kiuchumi.

Itakumbukwa juzi February 16 wakati wa maziko ya Msanii Godzilla, RC Makonda aliguswa kuahidi kutoa kiasi hicho cha fedha baada ya kugundua Marehemu Godzilla alikuwa na ndoto ya kumpatia mama yake mtaji wa shilingi milioni 5 kwaajili ya kufungua Pharmacy itakayomsaidia kuendesha maisha na tayari alikuwa ameshamkabidhi milioni 4 lakini baada ya Marehemu Godzilla kuugua ghafla Mama yake alilazimika kutumia fedha hizo kumuuguza mwanae na kusababisha fedha kuisha. 

RC Makonda amekabidhi kiasi hicho cha fedha mapema leo kwa Msanii Fareed Kubanda almaarufu kama Fid Q ili akiwakilishe kwa familia ya Marehemu Godzilla.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda(kushoto) akimkabidhi Msanii Fareed Kubanda almaarufu kama Fid Q(kulia) kwa niaba ya Mama Mzazi wa Marehemu Msanii Godzilla kiasi cha shilingi milioni 5 kama mtaji wa kufungua duka la kisasa la kuuza dawa za binadamu (Pharmacy).

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad