HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 19 February 2019

RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN AAENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYA YA KATI UNGUJA LEO

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Simai Mohammed Said, alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Maandalizi na Msingi Ng'ambwa Kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja Jimbo la Tunguu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, kushoto Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,wakisoma maelezo ya Jiwe la Msingi la Skuli ya Msingi na Maandalizi Ng'ambwa Uzi,Jimbo la Tunguu Zanzibar, baada ya kuondoa kipazia kuashiria uwekaji huo wa jiwe la Msingi la Jengo hilo la Madarasa, kulia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma.(Picha Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein kulia na kushoto Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma, wakipiga makofi baada ya hafla ya wekaji wa jiwe la Msingi la Skuli ya Msingi na Maandalizi  Ng'ambwa Uzi, Wilaya ya Kati Unguja Jimbo la Tunguu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,akiwahutubia Wananchi wa Kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja baada ya hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya Maandalizi na Msingi Ng'ambwa leo, akiendelea na ziara yake, kulia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheri.(Picha na Ikulu)
 WANANCHI wa Kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja Jimbo la Tunguu Zanzibar,wakifuatlia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, hayuko picha, baada ya hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Skuli ya Msingi na Maandalizi Ng'ambwa Uzi,leo akiwa katika ziara yake Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Ikulu)
 MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Ndg. Mussa Ramadhin Haji, akitowa taarafi ya upatikanaji wa Maji katika Kisiwa hicho wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, katika Kisiwa chac Uzi.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma, akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi Skuli ya Maandali na Msingi Ng'ambwa Uzi, wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, katika Wilaya ya Kati Unguja leo.(Picha na Ikulu)
KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Ndg. Mustafa Aboud Jumbe, akizungumza na Wananchi wa Kisiwa cha Uzi uimarishaji wa Miundombinu ya Ujenzi wa Barabara katika kisiwa hicho.(Picha na Ikulu)
 JENGO Jipya la Skuli ya Maandalizi na Msingi Ng'ambwa Kisiwa cha Uzi,  lililojengwa na Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Tunguu Zanzibar, na kuwashirikisha Wananchi wa Kisiwa cha Uzi, lililowekwa Jiwe la Msingi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein, akkiwa katika ziara yake katika Wilaya ya Kati Unguja leo.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad