HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 25 February 2019

MICHUANO YA CASTLE LAGER AFRIKA 5s ASIDE KUTIMUA VUMBI MEI 11

KAMPUNI ya bia ya Tanzania (TBL) kupitia bia yake yake ya Castle Lager wamezindua rasmi msimu  wa pili wa mashindano ya soka yanayoshirikisha wachezaji watano kila upande na mechi kuchezwa kwa dakika kumi katika mfumo wa bonanza ili kuweza kupata washindi, mchezo ujulikanao zaidi kama 5s Aside.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Meneja wa bia ya Castle Lager Pamela Kikuli amesema kuwa fainali za michuano hiyo zitahitimishwa rasmi Mei 11 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa hiyo ni mara ya pili ya kwa mashindano hayo kufanyika nchini ambapo awali yalifanyika katika nchi nyingine barani Afrika na mwaka uliopita Tanzania ilishiriki katika mashindano hayo katika kiwango cha kimataifa nchini Zambia.

Kikuli amesema kuwa mashindano ya mwaka huu yanatarajiwa kuwa bora zaidi yatakayotoa washindani wazuri na mabalozi katika mashindano ya kimataifa.

Kuhusiana na namna kupata timu zitakazoshiriki katika bonanza hilo Kikuli amesema kuwa mchakato umeboreshwa zaidi na washiriki watapatikana kupitia promosheni zitakazofanyika katika baa mbalimbali ndani ya jiji la Dar es salaam na kikosi cha promosheni hiyo kitatoa maelekezo ya namna ya kushiriki pamoja na kuunda timu zao.

Amesema kuwa lengo ni kuwafikia  wanywaji wa bia hiyo ya Castle Lager pamoja na kuwapa fursa ya kutimiza ndoto zao, na ameeleza kuwa mchakato wa kuhamasisha uundaji wa timuutafanyika katika baa 60 jijini Dar es salaam na kati ya hizo baa 32 pekee zitapata fursa ya kuunda timu zitakazoshirikikatika bonanza la fainali. Na ili kuingia 32 bora kigezo muhimu ni kufanya mauzo kwa wingi zaidi.

Kwa upande wake Balozi wa bia ya Castle Lager nchini Ivo Mapunda maandalizi mazuri yakifanywa Tanzania tuna nafasi kubwa sana ya kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa kwa mwaka huu.


Ivo amesema kuwa ushirikiano ukipewa nafasi kubwa zaidi nafasi ya kutwaa ubingwa wa Afrika  kwa mwaka huu ipo wazi kwa Tanzania kwa kuwa uzoefu ulipatikana katika michuano hiyo mwaka jana ambapo Zambia waliibuka kidedea.
Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli(katikati) akizungumza kwenye majadiliano ya  uzinduzi wa msimu wa pili wa msimu wa pili wa mashindano maalumu ya soka yanayofahamika kama ‘Castle Lager Africa 5s’ (5 – Aside kwa mkoa waDar es Salaam kutafuta timu ya Taifa. Kushoto ni Balozi wa Kampeni ya Castle Lager Africa 5s Tanzania, Ivo Mapunda.
Balozi wa Kampeni ya Castle Lager Africa 5s Tanzania, Ivo Mapunda akizungumza na waandishi wa habari wakati wa majadiliano ya uzinduzi  wa  msimu wa pili wa mashindano maalumu ya soka yanayofahamika kama ‘Castle Lager Africa 5s’ (5 – Aside) kwa mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli.
Balozi wa Kampeni ya Castle Lager Africa 5s Tanzania, Ivo Mapunda akipiga Penati kuashilia uzinduzi wa msimu wa pili wa mashindano maalumu ya soka yanayofahamika kama ‘Castle Lager Africa 5s’ (5 – Aside) yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli akipiga Penati kuashilia uzinduzi wa msimu wa pili wa mashindano maalumu ya soka yanayofahamika kama ‘Castle Lager Africa 5s’ (5 – Aside) yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja
Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa mashindano maalumu ya soka yanayofahamika kama ‘Castle Lager Africa 5s’ (5 – Aside).
Balozi wa Kampeni ya Castle Lager Africa 5s Tanzania, Ivo Mapunda akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa mashindano maalumu ya soka yanayofahamika kama ‘Castle Lager Africa 5s’ (5 – Aside).

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad