HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 25 February 2019

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA KALIUA NA URAMBO MKOANI TABORA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika uwanja wa Kolimba wilayani Kaliua, Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Picha iliyopigwa kutoka juu ikionyesha wananchi walivyojitokeza kwa wingi kwenye mkutano ambao Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Picha ya Jengo la Upasuaji lililojengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya halmashauri na michango ambalo limefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo wilayani Kaliua, Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisomewa taarifa ya mradi wa ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo cha afya Kaliua na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kaliua Dkt. John M. Pima .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria kukabidhiwa kwa zaidi ya pikipiki 15 kwa vijana wa boda boda ikiwa ni mkopo kutoka Halmashauri ya Kaliua, Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi hundi ya zaidi ya shilingi milioni 250 kwa vikundi 61 vya ujasiriamali ukiwa ni mkopo kutoka Halmashauri ya Kaliua, Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Sehemu ya wakazi wa Usoke Mlimani walioihudhuria mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Urambo mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu cha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika jimbo la Urambo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Margaret Sitta mara baada ya kuhutubia katika mkutano na wananchi wa kijiji cha Usoke Mlimani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad