HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 1 February 2019

KAMANDA MUROTO UNAYAONA HAYA?

Ndugu Mhariri nikiwa mmoja wa wakazi wa jiji la Dodoma napenda kutoa kero yangu kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwani nasikitishwa na vitendo vya kiuhalifu vinavyoendelea jiji hapa kwani imefikia hatua ya watu kuogopa kutembea zaidi ya saa nne kurudi katika nyumba zao katika baadhi ya maeneo.

Tunajua Mkoa wa Dodoma ni mkoa uliochaguliwa na Serikali kuwa makao makuu ya nchi na Julai 2016 Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alitangaza  rasmi Serikali yake kuhamia katika makao makuu hayo ya nchi.

Kwa sisi wageni wa Mkoa wa Dodoma tulifika na kujionea watu wenye wakarimu na upendo kwa wageni waotembela mkoa wao kwani tumeshuhudia shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania na shughuli nyingine za vyama na Serikali zikifanyika na kufana kwani ulinzi na usalama katika mkoa huu ulikuwa vyema.

Nakumbuka wakati  nikija kutembea Dodoma sikuwahi kusikia wizi wala ujambazi na nilishangaa kuona wakazi wa huku wengi wao wakiishi katika nyumba  zisizo na fensi na wengine kuyaacha magari yao yakiwa nje huku nikilinganisha na sehemu nilizowahi kutembelea katika miaka hiyo ikiwemo Arusha na Dar es Salaam kwani kuna wizi mkubwa wa magari ujambazi  wizi na uporaji wa vitu barabarani.

Suala la Serikali kuhamia Dodoma makao makuu ya nchi limekuja na masuala mazuri na maovu kwani sio watumishi wa Serikali pekee waliohamia kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma kutekeleza majukumu yao bali pia kuwa watu wasio na nia njema waliohamia Dodoma ili kusababisha wakazi wa Dodoma kukosa amani katika maeneo yao.

Uhamaji watu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine unakuja na tabia tofauti ikiwemo mila na desturi lakini katika hili la kuhamia Dodoma wengine wamehamia wakiona  kuwa ni fursa kwao kufanya vitendo vya kiuhalifu  hivyo kuleta taharuki kwa wakazi wenyeji na wageni katika katika eneo hili ambapo kabla vitendo hivyo havikuwepo kwa kiasi hicho.

Tumeshuhudia wizi wa televisheni za bapa katika maeneo tofauti ya jiji la Dodoma, kukabwa katika mitaa, uporaji kwa kutumia bodaboda na kubwa zaidi uvamizi katika nyumba kwa kutumia mbinu mbalimbali.

Niseme tu kuna vitendo vya wizi vimekuwa vikitokea na vingi vimekuwa vikiripotiwa Polisi ila bado vimekuwa vikiendelea kufanyika kwani kuna mtumishi wa Serikali ailiibiwa mara mbili televisheni nyumbani kwake, mwingine alivamiwa eneo la wajenzi na kuchomwa bisibisi na kuporwa vyote alivyokuwa navyo na mdada mmoja alivamiwa na majambazi nyumbani kwake mara baada ya wahalifu hao kufungua maji na yeye aliposikia  maji yanatoka alitoka  na kutaka kwenda kuyafunga ndipo walipoingia na kumjerui na panga mkononi na kuiba baadhi ya vitu.

Matukio mengi ya kiuhalifu yanayoendelea kutokea yanatufanya sisi wakazi wa Dodoma kuona kuwa hatupo sehemu salama.Tunaomba Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma chini ya Kamanda wa Polisi Gilles Muroto  kushirikiana na  wakazi wa Dodoma kuhimarisha ulinzi na usalama kwa raia na Mali zao ili kuufanya Mji huu mkuu wa Tanzania kuwa sehemu salama.

Ni Mimi Raymond Ishengoma  Mkazi wa Dodoma

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad