HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 9, 2019

UZALISHAJI WA SUKARI WAONGEZEKA TPC

Na Vero Ignatus, Kilimanjaro.
Kiwanda cha Sukari TPC kimeongeza uzalishaji wa sukari kutoka tani 36,000 ambayo ilikua ikizalishwa mwanzoni kabla ya ubinafsishaji na kufikia tani 110,000 ikiwa ni juhudi za kutatua changamoto ya upungufu wa sukari ya majumbani nchini ambayo ni tani 100,005.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Utawala kiwanda cha TPC ,Jaffari Ally alisema hayo katika ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba pamoja na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda katika kiwanda hicho ambapo alisema kuwa bado wanaendelea na upanuzi wa mashamba na wanatarajia kuzalisha tani 120,000 .

Jaffari aliipongeza serikali kwa kuziba mianya ya biashara magendo ya sukari ambapo sukari zisizokidhi viwango zilizua zikiingizwa nchini na kushindanishwa katika masoko ya ndani hivyo kuathiri viwanda vya ndani.

“Wazalishaji wa sukari tunapenda kuipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuzibiti mianya ya uingizwaji holela wa sukari ,miaka ya nyuma soko lilichafuliwa na sukari iliyokua ikiingizwa nchini isiyokua na viwango na iliingizwa kwa njia ya magendo bila kulipiwa kodi wala ushuru ,sukari ambayo ilikua ikiathiri afya za watanzania tunaishukuru serikali kwa kuziba mianya” alisema Jaffari

Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mghumba baada ya kutembelea kiwanda cha sukari cha tpc yakiwemo mashamba mapya ya miwa ,aliwataka wawekezaji hao kupanua wigo wa kilimo cha miwa ili kuongeza uzalishaji wa sukari .

Omari alisema kuwa kuna fursa kubwa ya uwekezaji katika mashamba ambayo yanastawi miwa yaliyopo katika mikoa ya Pwani,Kigoma,Musoma ambapo kuna maeneo makubwa ya uwekezaji.

Waziri wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda alisema kuwa bado kuna fursa kubwa ya uwekezaji katika sukari ya viwandani ambayo ina soko kubwa ili kupunguza wimbi la kuagiza sukari ya viwandani kutoka nje ya nchi.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda (kulia) na Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba wakiwa ameshika sukari inayozalishwa katika kiwanda cha TPC kufuatia ziara waliyoifanya katika kiwanda hicho jana.
Picha ya Pamoja ya Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda (kulia) na Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba wakiwa na uongozi nwa TPC,Bodi ya Sukari na Wataalamu wa Halmashauri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad