HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 23 January 2019

MKANDARASI ANAYESIMAMIA MRADI WA MAJI BOGA WILAYANI KISARAWE AONDOLEWA

 Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
 Mkandarasi wa Kampuni ya Mazongela Bulding Limited aliyekuwa anasimamia mradi wa Maji katika Kata ya Boga Wilayani Kisarawe ameondolewa kuendelea kusimamia ujenzi wa mradi huo baada yakubainika kusuasua kwa muda. 
 Kampuni hiyo ya ujenzi iliyo chini ya Mkandarasi, Salum Suleiman Ally ameondolewa kuendelea na ujenzi wa mradi huo licha yakutengewa zaidi ya Shilingi Milioni 536/- ambazo angelipwa katika utekelezaji wake. 
 Akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na Wananchi wa Kata ya Boga wilayani humo wakati akitembelea miradi mbalimbali ya Maji, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso amesema Mkandarasi huyo hafai kutokana na kuwaumiza Wananchi hao kwa muda mrefu, ambapo ameagiza asipewe kazi yoyote katika Halmashauri hiyo ya Kisarawe. 
 ‘’Changamoto kubwa katika Wilaya hii ya Kisarawe kuwaweka Wakandarasi wasio na uwezo kusimamia miradi mbalimbali ya Maji, wengi wanapatikana Kindugu hii haiwezekani’’, amesema Mhe. Aweso. Mhe. 
Aweso amewaasa Watendaji wa Wizara hiyo Wilayani humo, kukataa Wakandarasi wasio na uwezo, badala yake amewataka kuchukua Wandarasi wenye uwezo, hata hivyo Aweso amewataka Watendaji hao kuhakikisha Mkandarasi mwengine anapatikana kwa haraka ili kutekeleza mradi huo kwa haraka. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwangelo ameiomba Serikali kupitia Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso kuwachukulia hatua kali Wakandarasi ambao watashindwa kutekeleza miradi yao ipasavyo kutokana na Wilaya hiyo kukumbwa na kero kubwa ya Maji. 
 ‘’Kuna Miji mikubwa kama Nairobi imeundwa mwaka mmoja na Wilaya yetu lakini wao wana maendeleo sisi bado tupo nyuma’’, amesema Jokate. 
Naye Diwani wa Kata ya Boga, Inadi Chachaka amekili kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa Maji katika Kata hiyo, ambapo pia amemuomba Naibu Waziri kwa kushirikiana na Watendaji wake Wilayani Kisarawe kusimamia ipasavyo miradi hiyo ikiwemo Mradi wa Maji katika Kata ya Boga.
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwangelo akisisitiza jambo kwa Naibu wa Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso wataki walipotembelea mradi wa maji eneo la Mnarani, Kisarawe.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso pamoja na Watendaji wengine wa Wizara ya Maji wakiangalia mradi wa maji wa Kata ya Boga, Wilayani Kisarawe baada kuambiwa umesuasua kwa muda kutokana na Mkandarasi anayetekeleza mradi kushindwa kusimamia ipasavyo licha yakutengewa zaidi ya Shilingi Milioni 536/-
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso akishuhudia Shimo lililochimbwa kwa kile lilichoelezwa ni utekelezaji wa mradi wa maji, Kata ya Boga, Kisarawe.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwangelo wakimsikiliza Mhandisi wa Wilaya ya Kisarawe, Majid Mtili katika kutembelea utekelezaji wa mradi wa maji, Kata ya Chole.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad