HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 18, 2019

KIKAO CHA MAWAZIRI KUHUSU BOMBA LA MAFUTA KUFANYIKA KAMPALA WIKI IJAYO

Na Veronica Simba – Dodoma
Kikao cha Tatu (3) cha mawaziri wa sekta zinazohusika na utekelezaji wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), kinatarajiwa kufanyika Januari 25, mwaka huu jijini Kampala.

Kikao hicho kitakachotanguliwa na vikao ngazi ya wataalamu na baadaye ngazi ya makatibu wakuu wa Wizara husika, kitaongozwa na Mawaziri wenye dhamana ya nishati, ambao ni Dkt. Medard Kalemani (Tanzania) na Mhandisi Irene Muloni (Uganda).

Akizungumza jana, Januari 17, Makao Makuu ya Wizara ya Nishati jijini Dodoma, wakati wa kikao cha maandalizi kilichoshirikisha timu ya Tanzania inayohusika na usimamiaji wa utekelezaji wa mradi husika; Waziri Kalemani alitoa rai kwa wajumbe wote kufanya kazi kwa ushirikiano, kujituma na weledi wa hali ya juu ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati kwa faida ya Taifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, alisema anayo imani kubwa na kila mjumbe wa timu husika kwamba kuteuliwa kwao kuwa sehemu ya timu hiyo kumetokana na sifa zao kiutendaji na utaalamu, hivyo akawataka kutomwangusha Rais John Magufuli na Taifa kwa ujumla katika kutekeleza jukumu walilopewa.

Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, akichangia mjadala katika kikao hicho, alisema Ofisi yake imejipanga kutoa ushauri wote wa kisheria katika kuhakikisha mikataba mbalimbali inayoingiwa baina ya Tanzania na Uganda katika utekezaji wa mradi husika, inafuata misingi yote ya kisheria kwa manufaa ya Taifa.

Awali, akiwaongoza mawaziri, viongozi na wataalamu mbalimbali kupitia na kujadili ajenda za kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua alisema, hadi kufikia Desemba 2018, kazi mbalimbali za awali zimekamilika zikijumuisha tafiti za udongo, miamba na maji katika eneo la kituo cha kupokea, kuhifadhi na kusafirishia mafuta.

Aidha, alitaja kazi nyingine iliyokamilika kuwa ni tafiti za udongo, miamba na maji katika mkuza wa bomba pamoja na maeneo ya vituo vya Mradi; Stadi za mazingira na kijamii (ESIA); Tathmini za mali na utwaaji wa ardhi katika mkuza na maeneo ya kambi za utekelezaji Mradi pamoja na usanifu wa awali wa Mradi.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznia na Serikali ya Jamhuri ya Uganda zilisaini Mkataba wa makubaliano, Mei 26, 2017 ambao umeweka misingi ya utekelzaji wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

Tangu kusainiwa mkataba huo, Timu ya Majadiliano ya Serikali (GNT) imefanya vikao mbalimbali vya majadiliano na Timu ya Uganda katika miji ya Dar es Salaam na Arusha (Tanzania) pamoja na Kampala Uganda.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (mwenye miwani-katikati), akiongoza kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kulia kwake ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (mwenye miwani-katikati), akiongoza kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); (hawapo pichani) kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kulia kwake ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.
 Kutoka kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); (hawapo pichani) kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi, akifafanua jambo wakati wa kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); (hawapo pichani) kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mussa Sima wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); (hawapo pichani) kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, akiwaongoza mawaziri, viongozi na wataalamu mbalimbali (hawapo pichani) kupitia na kujadili ajenda za kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.e
Sehemu ya wajumbe wa kikao cha maandalizi kwa timu ya Tanzania inayotekeleza Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP); kabla ya kwenda Uganda kushiriki kikao cha majadiliano na Timu ya nchi hiyo, Januari 25, mwaka huu. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati, Dodoma, Januari 17, 2019.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad