HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 25 January 2019

BANDARI YAIFUNGA SIMBA NA KUTINGA FAINALI YA SPORTESA

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

TIMU ya Simba imekubali kichapo cha goli  2-1 toka kwa timu ya Bandari ya nchini Kenya kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Sportpesa.

Mechi hiyo ya nusu fainali ya kwanza ulikuwa n baina ya Bandari ya Kenya na Simba ambao mpaka dakika 90 mchezo huo unamalizikaBandari walifanikiwa kutinga hatua ya fainali.

Mchezo ulianza kwa Simba kuandika goli la kwanza katika dakika ya 44 kupitia kwa mshambuliaji wake wa Kimataifa Meddie Kagere na kuipeleka Simba mapumziko wakiwa kifua mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Bandari kutafuta goli la kusawazisha na katika dakika ya 58 Bandari wanapata penati inayofungwa na mchezaji William Wadri   na kupelekea matokeo kuwa 1-1.

Kwenye dakika ya 72, mchezaji Lugogo aliyeingia kwenye kipindi cha pili anaiandikia Bandari goli la pili akimalizia mpira ulipanguliwa na kipa Aishi Manula baada ya kupigwa Kona.

Mpaka dakika 90 zinamalizika Simba wanakuwa wameondolewa kwenye hatua ya nusu fainali na kwa sasa watakuwa wanasubiri timu itakayotolewa kwenye nusu fainali ya pili baina ya Mbai Fc na Kariobang na kucheza nae mshindi wa tatu.

Nusu fainali ya  michuano ya Sportpesa itachezwa siku ya Jumapili katika Uwanja wa Taifa ikifuatiw ana fainali itakayoanza majira ya saa 10 alasiri na mshindi wa mchezo huo atakutana na timu ya Everton ya Uingereza sambamba na kitita cha dola 30,000.
 Mchezaji wa timu ya Bandari William Wodry akijaribu kumtoka kiungo wa Simba James Kotei katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Sportesa iliyomalizika kwa Simba kuondolewa kwa jumla ya goli 2-1.
 Beki wa kati wa Simba Pascal Wawa akiwa amemtoka mchezaji wa Bandari Abdalla Hamis katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Sportesa iliyomalizika kwa Simba kuondolewa kwa jumla ya goli 2-1.


Golikipa wa Simba Aishi Manula akiwa ameruka juu na nkuudaka mpira uliokuwa umeelekzwa langoni mwake katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Sportesa iliyomalizika kwa Simba kuondolewa kwa jumla ya goli 2-1.

Wachezaji wa Bandari wakishangilia baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya fainali kwa kuwafunga Simba goli 2-1.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad