HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 25 January 2019

WAZIRI KIGWANGALLA ATUA NCHINI HAISPANIA, AUNGURUMA

Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla amewaita Wawekezaji kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii wakati aliposhiriki kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika.

Kongamano hilo limefanyika jana katika jiji la Madrid nchini Hispania
likiwa limeandaliwa na Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa (UNWTO)kwa
kushirikiana na Taasisi za Casa Afrika pamoja na Taasisi yamaonesho ya
Biashara ya Madrid (IFEMA) na kushirikisha nchi mbali mbali duniani.

Katika Kongamano hilo, Waziri Kigwangalla alipata fursa ya kuwa mmoja wa wazungumzaji ambapo amewahakikishia Wawekezaji wenye nia ya kuja kuwekeza nchini Tanzania kwamba ni sehemu salama ukizingatia hali ya amani na utulivu iliyopo nchini lakini pia kuna vivutio vingi vya utalii na fursa za kuwekeza.

"Nawakaribisheni nyote, Njooni Tanzania muwekeze kufuatia uwepo wa
mazingira na miundombinu bora kwa ajili uwekezaji katika sekta ya utalii
pamoja na viwanda" Alisema

Waziri Kigwangalla pia alitumia nafasi hiyo kwa kuutangaza ukanda mpya wa kusini mwa Tanzania ambao umejaliwa kuwa na vivutio vya Utalii vya kipekee vinavyopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mikumi pamoja Pori la Akiba Selous.

Katika hatua nyingine , Waziri Kigwangalla wakati akizungumza katika
kongamano hilo aliwaeleza washiriki hao kuhusu juhudi mbalimbali
zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Tanzania,John Pombe Magufuli kwa kutaja mifano michache kama vile kufufua kampuni yandege (ATCL) kwa kununua ndege mpya sita pamoja kujenga chanzo kikubwa cha kuzalisha umeme katika mto Rufiji.

Alisema serikali ya Tanzania pia inaendelea na mradi wa kisasa wa ujenzi wa njia mpya ya kisasa ya reli (Standard Gauge) pamoja na kuboresha
miundombinu ya barabara ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo.

Alibainisha kuwa kutokana na juhudi hizo zilizochukuliwa na Serikali hiyo,
sekta ya utalii itaweza kusonga mbele ikiwa pamoja na kurahisisha usafiri
kwa watalii pamoja na wawekezaji kwa ujumla.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa kongamano la 10 la Uwekezaji navBiashara katika sekta ya Utalii Afrika (Investour) lililofanyika Janakatika jiji la Madrid nchini Hispania ambapo katika Kongamano hilo WazirivKigwangalla alitumia fursa hiyo kuwaita Wawekezaji kuja nchini kwa ajili yavkuwekeza katika sekta ya Utalii na viwanda.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (mbele ) akiwa ni miongoni mwa washiriki akifuatilia kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika (Investour)  lililofanyika Jana  katika jiji la Madrid nchini Hispania ambapo katika Kongamano hilo Waziri Kigwangalla alitumia fursa hiyo kuwaita Wawekezaji kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii na viwanda.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiwa ni miongoni mwa Wazungumzaji  kwenye kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika (Investour) lililofanyika jana katika jiji la Madrid nchini Hispania ambapo katika Kongamano hilo Waziri Kigwangalla alitumia fursa hiyo  kuwaita Wawekezaji kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii na viwanda.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad