HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 25 January 2019

Naibu Waziri wa Afya Azindua bidhaa ya kikombe hedhi jijini Dar

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile akizungumza katika hafla ua uzinduzi wa bidhaa ya kikombe hedhi na teknolojia ya simu ya mkononi ya mzunguko wa hedhi iliyozalishwa na Kampuni ya AnuFlo Industries Ltd. Jijini Dar es Salaam
Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii 

NAIBU Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile amesema elimu ya hedhi bado ni changamoto hapa nchini, kwa sababu hakuna mfumo rasmi wa elimu hiyo na wengi hawaelewi kuhusu mzunguko.

Dk. Ndungulile ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa bidhaa ya kikombe hedhi na teknolojia ya simu ya mkononi ya mzunguko wa hedhi iliyoanzishwa na Kampuni ya AnuFlo Industries Ltd. Jijini Dar es Salaam

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema, elimu inatakiwa kutolewa ili kusaidia jamii kujua kuhusiana na mzunguko wa hedhi kwa sababu kuna baadhi ya wanafunzi wanakosa masomo wakiwa katika hali hiyo kwa kuhofia kuwa wapo tofauti na wengine.

Amesema,  elimu hiyo inatakiwa kutolewa kwa wanaume pia kwani nao wanapaswa  kuujua juu ya mzunguko huu, tusiishie kwenye mzunguko wa mpira tu," amesema Dk.Ndungulile
Amebainisha kuwa asilimia 50 ya watanzania wanaguswa na watoto hili hasa wasichana wenye umri  wa kati ya 15 hadi 18 asilimia 27 kwani  wengi wao ni wajawazito au ameshakuwa na mtoto.

 Amesema  takwimu Hizo ambazo hizo sio nzuri kwa nchi yetu, zimechangiwa zaidi na ukosefu wa elimu ya hedhi, na kuwashaurii kwa wadau mbalimbali waendelee kutoa elimu hiyo.


Aidha Dk. Ndungulile ametaja changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya hedhi salama kuwa bado ni kubwa kiasi ambacho mtu anaweza kupata maambukizi ya maradhi kama hajatumia vifaa salama.

"Mimi kama daktari nalielewa sana jambo hili kwa upana, linaashilia kuwa kijana amepevuka na linaumuhimu katika ukomo wa hedhi, ambapo ndiyo mwisho wa kupata mtoto, kwa hiyo elimu hii ni muhimu kwa kila mmoja," alisema Dk.Ndungulile

Ameongeza kuwa,  wakitokea wajasiliamali kama hawa tunahakikisha tunawashika mkono  kuhakikisha wanatimiza malengo yao.
Naye,  Mkurugenzi wa Kampuni ya Anuflo, Flora Njelekela amesema tafiti za hedhi salama nchini zinaonesha, kuwa asilimia 65 ya wanawake nchini kupata hedhi kila mwezi huku asilimia 82 ya Wasichana na wanawake akiwa hawana uelewa juu ya afya na hedhi salama.

Amesema, ukosefu bidhaa hedhi salama hulazimisha msichana mmoja kati ya 10 kukosa masomo kwa siku tatu hadi tano kila mwezi ambazo ni sawa na asilimia 20 ya siku za masomo kwa mwaka.

Njelekela amesema  kutokana na uhaba wa bidhaa hizo,  garama takwimu, na tafiti zilizofanywa kuhusiana na hedhi salama ndiyo maana Kampuni yake ikajikita katika kuzalisha kikombe cha hedhi, kwa sababu ni salama ni hakina madhara, kinadumu kwa muda mrefu na Pia kitawafanya wanafunzi wasome kwa raha.

Alisema kikombe hedhi hicho,  kimekuja kukabiliana na tatizo la uchafuzi wa mazingira, kwa sababu kitatumika kwa kipindi cha miaka mitano na  pia kinawekwa kwa masaa 12 asubuhi hadi jioni ndiyo mtu anakitoa.
Mkurugenzi huyo amesema hiyo imetengenezwa kwa kuzingatia ubunifu makini na teknolojia za kisasa kwani kimetengenezwa kwa asilimia 100 ya LFGB medical silicone ambayo haileti Madhara 

Kwa upande wake, Muwakilishi wa Ofisa  Elimu Mkoa, Maimuna Mtanda amesema kikombe hicho kitaondoa suala la utorosho shuleni , sio kwamba wanafunzi hawapendi kwenda shule ni kutokana na kutokuwepo na mazingira rafiki ya wao wakiwa kwenye hedhi.


Naye, Dada Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana, Jangwani, Jackline Shio alisema walikuwa wanapata changamoto katika kipindi cha hedhi , kutokana na gharama za taulo za kike kuwa kubwa ila Flora ameweza kulitatua tatizo hilo kwa kuwaletea kikombe cha hedhi.

Mwanafunzi huyo alitoa pendekezo kuwa elimu hiyo iendelee kutolewa ili kuokoa wanafunzi wanaokosa masomo, kipindi ambacho wanakuwa na hali hiyo.No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad