HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 1, 2018

WAZIRI MHAGAMA AAGIZA UONGOZI WA NSSF KUWA NA UZALENDO KATIKA UTENDAJI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Waziri Mhagama ameuagiza uongozi wa Shiriki la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kubadili mitazamo dhaifu ya kiutendaji na kuanza kufanya kazi kwa kuongozwa na uzalendo ili kuleta tija na kufikia malengo ya Shirika hilo.

Ametoa kauli hiyo mapema mwishoni mwa wiki hii (Novemba 29, 2018) alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi inayoratibiwa na shirika hilo ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu Dar es Salaam. Maeneo aliyotembelea ni pamoja na; miradi wa nyumba za bei nafuu za Dungu, Mtoni Kijichi, Tuangoma na Mzizima pamoja na nyumba za Dege Beach Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Kauli ya waziri imekuja mara baada ya kutoridhishwa na hali ya maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo na kuuagiza uongozi wa Shirika hilo kubadili mitazamo ili kuwa na malengo yanayotekelezeka na kwa wakati. “Kwa muda mrefu mmekuwa mkifanya kazi kwa kujitenga katika makundi, mnapaswa kubadili mitazamo hasi na kuwa na mitazamo chanya yenye utendajikazi katika hali ya umoja ili kuendelea kubadili NSSF ili iwe na uzalizaji wa tija”.alieleza Mhagama

Waziri aliongezea kuwa Shiriki linapaswa kubadili hali za mazoea yaliyokuwa si mazuri ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano iliyojikita katika uwajibikaji wa kizalendo. “Lazima mbadili mitazamo ya uongozi  wa mazoea na kuanza kufanya kazi kwa umoja ili kuwa na matokeo chanya yanayokusudiwa ili kuwa na tija kwa jamii na Serikali kwa ujumla”.Alisisitiza Mhagama

Sambamba na hilo waziri alielekeza uongozi wa NSSF pamoja na bodi  kuanza kuchukua hatua kwa watendaji wazembe pasipo uwoga katika kuongoza kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

“Niwaombe Uongozi wa Shirika pamoja na Bodi mfanye kazi mkiongozwa na sheria, kanuni na taratibu zilizopo, mahali pa kuchukua sheria, tuone mkifanya hivyo bila kuoneana aibu”.Alisisitiza Waziri. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi za Jamii wa NSSF Bw.William Erio aliahidi kuchukua maelekezo ya waziri kwa vitendo na kuanza utekelezaji wa haraka juu ya maeneo aliyoelekeza.

“Niahidi kwa kushirikiana na menejimenti na bodi kuendelea kuweka mipango inayotekelezeka na kuhakikisha tunawajibika ili kuwa na NSSF yenye sura mpya”.Alisema Erio. Naye mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya mfuko huo Balozi Ali Iddi Siwa aliahidi kutekeleza maagizo yaliyotolewa na kuhakikisha waneendelea kuhakikisha shirika linakuwa katika viwango vya juu kama matarajio ya Serikali juu ya NSSF.

“Nikuhakikishie kuwa tutafanya yale yote uliyoagiza ili kuendelea kulitangaza vyema Shirika  na kuhakikisha kazi zote za Bodi zinatekelezwa vyema kwa kuzingatia utawala bora wenye weredi na uzalendo”.Alisisitiza Balozi.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama akiuliza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw.William Erio wakati wa ziara yake katika mradi wa ujenzi wa nyumba za Denge Beach Kigamboni Jijini Dar es Salaam Novemba 29, 2018.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama akiangalia ramani ya ujenzi wa mradi wa Dege Beach Kigamboni uliojengwa na Shirika la Mifuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF Dar es salaam, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi huo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama akiuliza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw.William Erio (mwe nye koti la kijivu) wakati wa ziara yake eneo la Dungu lenye nyumba 439 ambapo tayari nyumba 94 zimekamilika katika eneo hilo.
 Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF Bi Jayne Nyimbo akitoa maelezo ya ufafanuzi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama wakati wa ziara yake katika mradi wa nyumba za Dege Kigamboni Dar es Salaam.
 Mhandisi Masuhuko Nkuba akitoa ufafanuzi wa ujenzi wa mradi wa ghorofa 35 za Mzizima Tower kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama wakati wa ziara yake.
 Muonekano wa baadhi ya majengo ya mradi wa nyumba za bei nafuu za Tuangoma zilizojengwa na Shirika la NSSF zilizopo Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama akiangalia urefu wa jengo la Ghorofa 35 la Mzizima wakati wa Ziara yake kukagua maendeleo ya mradi wa nyumba za NSSF Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho pamoja na Uongozi wa NSSF na Bodi ya Wadhamini wa Shirika hilo mara baada ya kumaliza ziara yake Dar es Salaam.
Wajumbe wakifuatilia maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Waziri Mhagama (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad