HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 20, 2018

WADAU WA JINSIA WAKUTANA MJINI MOROGORO KUFANYA MAPITIO SERA YA TAIFA YA JINSIA

Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii inakutana na wadau wa masuala ya Jinsia kujadiliana na kufanya mapitio ya sera ya Taifa ya Jinsia ili pamoja na mambo mengine iweze kuwa na masuala ya wanawake waishio vijijini lakini pia kuzingatia makundi mengine maalumu hususani vijana na watu wenye mahitaji maalum.

Akiongea wakati wakufungua kikao kazi na wadau wa sera ya jinsia kutoka Wizara za serikali na mashirika yasiyo ya Kiserikali Kaimu Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara kuu Maendeleo ya Jamii Bi Grace Mbwilo amewataka wadau hao kufanya mapitio ya sera hiyo lakini pia kuangalia namna bora ya kutatua changamoto zinazomkabili mwanamke wa kijijini.

Aidha Bi. Mbwiro pia amewataka wadau hao kuangalia masuala mengine katika jamii akisema ni mengi mno hivyo kuzingatia vipaumbele vya masuala ya jinsia kwa wanawake  akisema kundi hilo katika jamii bado linachangamoto ambazo zinalifanya kuendelea kubaki katika nyanja tofauti.

‘’Sote tunajua kuwa wanawake wengi zaidi wanatoka maeneo ya vijijini hivyo ni vyema mnavyofanya mapitio katika sera hii kuzingatia namna bora ya kumaliza au kumsaidia mwanamke wa kujijini kuondokana na chanagamoto hizo.” Aliongeza Bi.Grace Mbwilo.

Wakati huo Afisa dawati anayeshugulikia mapitio ya sera ya Taifa ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Dora Neema amewambia wadau hao kuwa mchakato wamapitio ya sera hiyo ulianza toka mwaka 2006 na kupitia kwa wataalami washauri ambao kwa nyakati tofauti walitoa mapendekezo ya kuboresha sera hiyo hivyo wadau watayaangaria maboresho hayo na kuyazingatia wakati wa mapitio ya sera hiyo.

Sera ya Taifa ya Jinsia inapitiwa na wadau ili kurekebisha mapungufu yaliyopo  pia kuboresha sera hiyo  ili niweze kukidhi  matakwa ya kijinsia kwa makundi yote ya kijamii ikiwemo vijana, wanaume pamoja na watu wengine wenye mahitaji maalumu bila kumweka kando mwanamke anayeishi kijijini.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi Grace Mbwilo katikati akiongea na wadau mbalimbali wa masuala ya Jinsia wakati wa  kujadiliana na kufanya mapitio ya sera ya Taifa ya Jinsia leo Mkoani Morogoro.
 Wadau mbalimbali wa masuala ya Jinsia wakati wa  kujadiliana na kufanya mapitio ya sera ya Jinsia katika kikao  kikazi cha wadau wadau wa Jinsia kinachoratibiwa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maeandeleo ya Jamii leo Mkoani Morogoro.
 Wadau mbalimbali wa masuala ya Jinsia wakati wa  kujadiliana na kufanya mapitio ya sera ya Jinsia katika kikao  kikazi cha wadau wadau wa Jinsia kinachoratibiwa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maeandeleo ya Jamii leo Mkoani Morogoro.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa masuala ya Jinsia wakati wa  kujadiliana na kufanya mapitio ya sera ya Jinsia katika kikao  kikazi cha wadau wadau wa Jinsia kinachoratibiwa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maeandeleo ya Jamii leo Mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad