HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 19 December 2018

RC Wangabo atoa tahadhari ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kalambo

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa tahadhari kwa uongozi wa wilaya ya Kalambo juu ya matumizi na ubora wa hospitali inayotarajiwa kujengwa katika wilaya hiyo ili kusijirudie makosa yaliyofanyika wakati wa ujenzi wa vituo vya afya vinavyoendelea ikiwemo kuchelewesha malipo kwa mfundi pamoja na kuachana na mafundi wasumbufu wanaochelewesha ujenzi.

Akitolea mfano wa ujenzi wa kituo cha afya cha Legeza Mwendo kilichopewa Shilingi milioni 700 na hatimae kufanikiwa kujenga majengo tisa, hivyo kumtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwa usimamizi wa mkuu wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanazitumia vyema Shilingi bilioni 1.85, fedha ambazo zimetengwa na serikali kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya.

“Utoaji wa fedha ofisi yako Mkurugenzi mmekuwa mnasuasua, malipo mnasingizia sijui mifumo mifumo, watu hawalipwi kule (kituo cha afya) Mwimbi imekuwa tabu karibu mwaka mzima, hata kule (kituo cha Afya) Legeza mwendo ilikuwa hivyo hivyo, nisingependa hili litokee, malipo lazima yaende vizuri, hata wale mama lishe walikuwa wanadai hawalipwi,” Alisisitiza.

Alisema kuwa kutokana na fedha hiyo iliyotengwa angependa kuona majengo mazuri yenye viwango ili kuupendezesha mji wa Matai ambao ni makao makuu ya wilaya hiyo.

Maeyasema hayo katika ziara yake ya kuona maazimio ya eneo la ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kalambo ambapo kumekuwa na mvutano juu ya eneo la kuijenga hospitali hiyo huku maeneo kadhaa yakihitaji fidia wakati maelekezo ya fedha hizo si kwa nia ya kulipa fidia bali ni ujenzi huku zikiwa zimebaki siku chache Ofisi ya Rais TAMISEMI kurudisha fedha zake endapo fedha hizo zitakuwa hazijaanza kutumika kwaajili ya ujenzi uliokusudiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mh. Daudi Sichone alimshukuru Mkuu wa mkoa kwa msukumo wake wa kusimamia miradi hiyo ya maendeleo pamoja na kuwasukuma wafanye haraka kutafuta ufumbuzi wa ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya ili wananchi waweze kupata huduma bora na kwa wakati.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad