HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 19, 2018

MBIO ZA HEART MARATHON MWAKA 2019 KUAMBATANA NA UPIMAJI WA AFYA

 Rais wa Taasisi ya  Tanzania Health Summit (THS) Dkt. Omary Chillo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na msimu wa mbio za Heart Marathon kwa mwaka 2019 na kueleza kuwa tangu kuanza kwake 2016 zaidi ya watu 3000 wamekimbia na watu 1000 wamefanyiwa vipimo vya magonjwa yasiyoambukizwa leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu mkuu msaidizi wa Chama cha riadha Tanzania bi. Ombeni Zavala akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mbio za Heart Marathon ambazo zitafanyika mapema Aprili mwaka 2019, na kusema kuwa THS wawe mfano wa kuigwa hasa kwa kuhamasisha umma kufahamu na kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, leo jijini Dar es Salaam.
 Wawakilishi kutoka Nexlaw Advocate wakikabidhi hundi ya fedha ya shilingi milioni 7 kwa waandaaji wa mbio za Heart Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 28, 2019 wakti wa mkutano wa waandishi wa hari uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii)

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
TAASISI ya Health Summit (THS) kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na shirika la Save the Chirldren Tanzania kwa mara ya nne, wameandaa mbio za Heart Marathon kwa mwaka 2019 ili kuhamasisha jamii kupambana na magonjwa yasiyoambukiza na kuongeza nguvu katika juhudi za serikali za kukabiliana na magonjwa hayo ikiwa ni pamoja na kuchangia fedha kwa watoto wenye matatizo ya moyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 19. 2018 jijini Dar es salaam kuhusiana na mbio hizo Rais wa Tanzania Health Summit Dkt. Omary Chillo amesema lengo kubwa la mbio hizo ambazo zitafikia kilele Aprili 28, 2019 katika viwanja vya Coco Beach ni kusaidia juhudi za serikali za kupunguza magonjwa yasio ya kuambukiza kwa kupitia michezo na kuchangia fedha kwa ajili ya watoto wanaohitaji upasuaji katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Chillo amesema kuwa, "Mbio za Marathon 2019 zitaambatana na mambo mengine ikiwa ni pamoja na kupanua uelewa juu magonjwa yasiyoambukiza mathalani kisukari, shinikizo la juu la damu na unene kupita kiasi na kudumisha afya bora kupitia mazoezi na utoaji wa ushauri kuhusu lishe bora, upimaji wa afya pamoja na kutoa burudani kwa wananchi" ameeleza Chillo.

Aidha amesema kuwa zawadi zitakazotolewa ni pamoja na fedha taslimu zenye jumla ya thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16 kwa wakimbiaji watakaokimbia mbio za kilomita 21, kilomita 5 na mita 700 kwa watoto na ameziomba taasisi mbalimbali nchini kuchangia na kushiriki katika mbio hizo kupitia tovuti yao ya www.heartmarathon.com ili kuweza kuokoa maisha ya watoto na wananchi kutoka katika janga la magonjwa yasiyoambukizwa.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete Dkt. Naiz Majani amesema kuwa wanaungana na taasisi ya Tanzania Health Summit katika mbio hizo ili kuweza kuwachangia watoto wenye matatizo ya moyo kuweza kupata matibabu.

Dkt. Majani amesema kuwa kuanzia mwaka 2015 matibabu ya moyo yalianza kufanyika hapa nchini na hasa katika masuala ya upasuaji na hadi kufikia sasa jumla ya watoto 1040 wamepata matibabu ambapo watoto 600wamefanyiwa upasuaji mkubwa na zaidi ya watoto 400 wamefanyiwa upasuaji mdogo.

Pia amesema kuwa serikali imejipanga katika kuhakikisha matibabu yanatolewa nchini na hadi sasa wameshapatiwa wodi maalumu kwa ajili ya matibabu ya watoto pekee.

Naye katibu msaidizi wa chama cha riadha nchini bi. Ombeni Zavala amewapongeza THS kwa kuandaa mbio hizo kwa malengo ya kuwasaidia waatoto wenye matatizo ya moyo na kuelimisha umma kuhusiana na magonjwa ya yasiyo ya kuambukiza na ametoa wito kwa waandaaji wa Marathon kote nchini kufuata kanuni hasa katika suala la ugawaji wa zawadi kwa wanawake na wanaume.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad