HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 19 December 2018

BATA WAPEWE THAMANI KAMA JAMII ZINGINE ZA NDEGE ILI KULETA UFUGAJI WENYE TIJA

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii

UMOJA wa wafugaji bata nchini wamekutana na kuzindua tamasha la uchomaji wa  nyama ya Bata  katika ukumbi wa police officers mess jijini Dar es salaam.

Akifungua hafla hiyo ya tamasha la uchomaji nyama ya bata Afisa mifugo wa jamii ya ndege Deodratus Nestory kutoka Manispaa ya Kinondoni  
 amewapongeza  wafugaji hao na kusema kuwa ni   nadra sana kukuta tamasha la uchomaji nyama ya bata kwani imeshazoeleka mbuzi choma na kuku choma.

Nestory amesema kuwa "Umoja huu upo kwa ajili ya  kutia watu hamasa ili waweze kutambua thamani ya nyama ya bata, na Manispaa ya Kinondoni itatoa semina kwa wafugaji wote wa mbuzi,ngombe, kuku na bata ili waweze kupata masoko kwa urahisi na  kuwapa ushirikiano kutoka Serikalini kuanzia Manispaa hadi Wizara husika ya Kilimo na ufugaji" amesema Nestory.

Pia Nestory amefafanua kuwa kufikia mwakani  watafungua chama cha wafugaji wa jamii ya ndege ambacho kitatambulika kisheria
Ili waweze kupata mkopo kutoka mabenki tofauti na kuwawezesha kupanua soko na ufugaji wenye tija.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyowakutanisha wafugaji wa Bata kutoka sehemu mbalimbali yakiwemo Kawe, Kibiti,Morogoro,kigamboni na Bunju  Mwenyekiti wa chama hicho Riziki osward amesema sasa ni wakati wa kumpa thamani bata pamoja na nyama ya bata kwani jamii bado haina mwamko katika Kula kwa wingi nyama hiyo.

Hata hivyo osward amefafanua zaidi kuwa lengo la tamasha hilo sio tu Kula nyama peke yake bali hata kujifunza  namna bora ya kufuga bata hao hasa katika kuanzia malisho ,madawa na chakula.

Pia ameeleza kuwa mikakati ya Umoja wa wafugaji bata itahakikisha inatoa elimu kwa wafugaji na kuwasaidia ili kuweza kupanua soko na kumpa thamani bata kwani bado kuna desturi iliyojengeka juu ya bata kuwa ni mchafu japo bata ana thamani kubwa kuliko kuku .

Amesema kuwa "Tujikite katika ufugaji wa bata kwani unaweza ukaanza na jike moja ambalo kwa kawaida unaweza kupata kwa elfu 30 na baadae unaweza ukaingiza pesa nyingi ambapo itakukwamua kiuchumi " alisema Riziki 

Kwa upande wa mmoja wa wafugaji bata Henry Henry ameeleza changamoto zinazowakumba  ni kukosa mitaji pamoja na usimamizi mzuri katika kuleta mabadiliko ya ufugaji wa kisasa na ameomba  kuwepo kwa Afisa mifugo ambaye ataweza  kutoa elimu na kuhakikisha magonjwa vamizi yanapatiwa suluhishopamoja na kutoa ushauri jinsi ya ufugaji wenyewe tija.

Ameeleza kuwa "Hata hivyo  kwa sasa serikali ya awamu ya tano kupitia Rais John Pombe Magufuli Katika kutekeleza sera ya hapa kazi tu  anaunga mkono vijana na kuhusiana na suala la wafugaji bata ninaamini litapewa kipaumbele ili kuongeza pato la Taifa "amesema Henry.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad