HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 7, 2018

Manyanya : OSHA kazi yenu inaonekana kila sehemu

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa Wakala wa Afya wa Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) kazi yao inaonekana kila sehemu ya viwanda wanamuambia Usalama kwanza kwa kupata vifaa ni kisha kuingia. Manyanya  ameyasema hayo wakati alipotembelea banda la OSHA wakati alipotembelea banda la OSHA katika maonesho ya Tatu ya bidhaa za viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam amesema kuwa OSHA wamefikisha elimu kwa wenye viwanda na sehemu zingine juu ya usalama mahala pa kazi.

Amesema kuwa viwanda vyote alokopita wamejizatiti katika usalama wa wafanyakazi wao kwa kuwa na vitu vya usalama kuanzia nje hadi ndani katika mitambo. Aidha amesema kuwa OSHA waendelee na utoaji elimu kila siku katika kulinda Afya na madhara mengine katika sehemu za kazi.

Nae Afisa Habari wa OSHA Eliuter Mbilinyi amesema wamekuwa wakitoa elimu ya Afya katika sehemu mbalimbali katika kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa salama. Amesema OSHA  lengo kubwa ni kuwalinda wafanyakazi katika vifo pamoja na madhara mengine yanayotokana na mitambo. Amesema Viwanda ni wadau muhimu ambao wanatakiwa kuzinagatia kanuni na viwango katika sehemu ya kazi pamoja na kufanyiwa usajili.
 Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya akizungumza katika banda la OSHA wakati alipotembelea maonesho ya Tatu ya bidhaa za viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Wananchi wakipata huduma katika banda la OSHA katika maonesho ya Tatu ya bidhaa za viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa mwananchi akipata huduma katika la Wakala wa Afya wa Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) wakati alipotembelea banda la OSHA katika maonesho ya Tatu ya  bidhaa za  viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya da Sabasaba jijini Dar es Salaam. 
Afisa Habari wa mwaka Wakala wa Afya wa Usalama Mahala pa Kazi OSHA Eliuter Mbilinyi akizungumza na waandishi habari katika maonesho ya Tatu ya bidhaa za viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad