HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 12, 2018

BITEKO AICHARUKIA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI KIJIJI CHA MANGAE , WILAYANI MVOMERO

Na Mwadishi wetu, Morogoro
NAIBU Waziri wa Madini, Doto Biteko ameiagiza Menajimenti ya Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji ch  Mangae  wilayani Mvomero, mkoani Morogoro kusimamisha uchimbaji  hadi itakapokamilisha taratibu za kisheria za Serikali  zinazosimamia madini  pamoja na kuwalipa fidia wananchi waliohamishwa meneo yao  waliokuwa wakiishi.

Biteko alitoa agizo hilo baada ya kufanya ziara  ya kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo kwenye  eneo la mgodi huo uliopo katika vijiji vya Mtupule na Mangae  na  kubaini imekuwa ikeindelea kuchimba madini  ya dhahabu kinyume na sheria  licha ya kutakiwa kukamilisha kwanza  utaratibu waliopewa wa kisheria .

Mbali na hilo , Naibu Waziri alionya na kutoa wito  kwa Watanzania wote wanapoamua kuingia mikataba na mikataba ya  wachimbaji wadogo ni lazima itambuliwe na serikali kwa mujibu wa sheria ya uwekezaji  sekta ya madini na si vinginevyo.

Naibu Waziri alisema , kufuatwa kwa sheria na  utaratibu wa mikataba na wawekezaji wa n je inalenga kuwalinda   uwekezaji wao  ili  baadaye wasione wananyanyaswa pale  mikataba walioingia na watu wasio waaminifu inakinzana na sheria mpya  ya  madini

Hata hivyo alisema ,  manufaa ya madini kwa wananchi wa eneo hilo hayawezi kupatikana  endapo mahusiano kati ya mgodi na wananchi hayatakuwa mazuri na kwamba  rasilimali za nchi lazima ziwanufaishe Watanzania  wote yakiwemo Madini.

“ Wizara ya Madini inatoa leseni  na mwenye leseni baada ya kuipata anapaswa kwenda kujitambulisha kwa Mkuu wa wilaya husika  na mkuu wa wilaya anamtambulisha kwa mtendaji wa Kata hadi   Kijiji “ alisema Biteko na kuongeza kusema

“ Kwa pamoja watendaji wa kata na kijiji wataenda kuweka alama ya mipaka eneo la uchimbaji na kukiwa  na watu juu ya ardhi na mimea yao hapo mwekezaji atafanya mazungumzo  na wananchi ili kuwalipa  fidia kulingana na utaratibu wa kisheria wa uthamini kabla ya  kuanza uchimbaji ” alisema Biteko.

Naibu Waziri huyo alisema ,kwa mujibu wa sheria hakuna mtu mwenye leseni kuchimba madini bila kumalizana na mtu aliyemkuta juu ya ardhi ,hivyo alimwagiza mkuu wa wilaya ya Mvomero kwa kushirikiana na mamkala zingine kuhakikisha shughuli za uchimbaji hazifanyiki hadi wananchi watakapolipwa fidia zao ikiwa na kukamilisha sheria za madini.

 Nao baadhi ya wananchi wa  vijiji hivyo waliokusanyika eneo la mgodi baada ya kuwasili Naibu Waziri  kwa nyakati tofauti walitoa malalamiko yao  dhidi ya mwekezaji huyo ikiwemo ya kufunga barabara inayiunganisha vijiji vyao na makao makuu ya kata ambayo  inapita  eneo la mgodi.

Baadhi ya wakazi hao akiwemo Mchungaji wa  Kanisa la Methodist, Hilda Ngowi ,  Anista John , Andrian Soketi pamoja na  Karaita Saita kwa nyakati tofauti  wakidai mbele ya Naibu Waziri huyo kuwa  mwekezaji huo wamewaondoa maeneo hayo bila kuwalipa fidia na kuanza shughuli za uchimbaji wa madini.

Hata hivyo alidai ,baadhi ya wananchi walilipwa  fedha kidogo kiwango kinachofikia  Sh 500,000 na bati 23 tu jambo ambalo halikuwa la kisheria .

Mchungaji  Ngowi ,alilamikia kwa mwekezaji huyo  kufunga barabara hali inayowawia vigumu wao kusafiri kutoka upende mmoja wa vijiji hivyo ikiwa ni kwenda kupata huduma za matibabu  Zahanati iliyopo makao makuu ya Kata na  vijana wazawa kukosa ajira.

Naye mkuu wa wilaya hiyo, Utaly alisema, tayari walianza kuchukua hatua kabla ya ujio wa Naibu Waziri hasa la matumizi ya barabara na kwamba kufuatia maaagizo hayo , Serikali ya wilaya itasimamia utekeleaji wa kuona fidia inalipwa kwa wahusika  na barabara inafunguliwa na kuwataka wananchi kufuata utaratibu rafiki utakaowekwa wakati wa kupita eneo la mgodi huo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni ya MMC , Daniel Agustino alisema kuwa kampuni huyo ilipata usajili wake  Novemba 2015 na kuanza shughuli za utafutaji wa nmadini mwaka 2016 katika kijiji cha Mangae , Kata ya Mangae , wilayani Mvomero.

Hata hivyo alisema kuwa,  changamoto zote ziliozjitokeza na maelekezo ya Naibu Waziri wa Madini yatatekelezwa kwa haraka ili shughuli za uchimbaji ziweze kuruhusiwa tena kwa manufaa ya Kampuni, jamii  na taifa kwa ujumla.
 Mkazi wa kijiji cha Mangae , kata ya Mangae, wilayani Mvomero mkoani Morogoro, Anita John  akitoa malalamiko yake  kwa Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko ( hayupo pichani )  kuhusu  Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa  dhahabu  katika eneo la kijiji hicho kuendesha shughili zao pasipo kuwafidia  makazi yao  waliyokuwa wakiishi kupisha uchimbaji wake.
 Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  akisoma  baadhi ya nyaraka za  Kampuni ya MMC  ya  uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae  wilayani Mvomero, mkoani Morogoro  wakati wa  ziara ya  kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo na ( wapili kulia) ni Mkuu wa wilaya hiyo, Mohamed Utaly.
 Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  ( aliyeweka mikono mfukoni) akipewa maelezo na kuangalia mashine  za  Kampuni ya MMC zilizofungwa kwenye mgodi wa uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae  wilayani Mvomero, mkoani Morogoro  wakati wa  ziara  ya kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo.
 Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  ( aliyeweka mikono mfukoni) akiteremka chini kutoka kuangalia mashine  za  Kampuni ya MMC zilizofungwa kwenye mgodi wa uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae  wilayani Mvomero, mkoani Morogoro   wakati wa ziara  ya kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo.
 Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  ( mwenye kuvaa shati la madoamadoa ) na ( wa  kawanza kulia ) ni  Kamishina  kutoka Tume ya Madini , Dk Athanas Macheyeki , na ( wapili kushoto ) ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero ,  mkoani Morogoro  , Mohamed Utaly  pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa  Kampuni ya MMC  ya uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae   wakazi wa ziara ya  kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo.
 Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  ( wapili kulia ) akiongozwa na Mwakilishi wa  Kampuni ya MMC  ya uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae , wilayani Mvomero , mkoani Morogoro,  Daniel Agustino  ( kulia) ambaye pia ni mhasibu wakazi wa ziara ya  kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo wengine walioambatana na Naibu Waziri ( kati kati mstari wa nyuma ) ni  mkuu wa wilaya hiyo , Mohamed Utaly .
  Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  ( kulia  ) akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya MMC  ya uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae ,  wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro  wakati wa   ziara  ya kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo na ( kati kati mwenye kushika simu) ni mkuu wa wilaya ya Mvomero, Mohamed Utaly.
  Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  ( kushoto ) akiwahoji jambo baadhi ya wafanyajkazi waliopo kwenye Menejimenti ya  Kampuni ya MMC  ya uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae ,  wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro wakiongozwa na Mwakilishi wa uongozi wa juu wa Kampuni  wake Mwakilishi wa Kampuni ya MMC ,  Daniel Agustino  ( kulia) ambaye pia ni mhasibu  wakati wa ziara  ya kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo .
Wakazi wa  vijiji vya Mangae , Msongozi  na Mtipule   katika kata ya Mangae, wilayani Mvomero mkoani Morogoro, wakitoa  malalamiko yao  kwa Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko ( hayupo pichani )  kuhusu  namna ya Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa  dhahabu  katika eneo la kijiji hicho isivyowatendea haki kwa kushindwa kwao kuwalipa fidia , kufunga barabara na ajira za upendeleo kwa wageni  wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za Kampuni hiyo.
 Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  ( wapili kutoka kulia  ) akisikiliza kero na changamoto mbalimbali za wakazi wa vijiji vya Mangae , Msongozi  na Mtipule  vilivyopo wilaya ya Mvomero , mkoani Morogoro  dhidi ya  Kampuni ya MMC  ya uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae  wakati wa  ziara  ya kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo na  ( watatu kulia) ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero , Mohamed Utaly  na ( wa kwanza kulia anayeandika ) ni Kamishina  kutoka Tume ya Madini , Dk Athanas Macheyeki.
  Baadhi ya watendaji wa menejimenti ya wafanyakazi wa Kampuni ya MMC  ya uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae ,  wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro  wakimsikiliza Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  ( hayupo pichani  ) katika kikao kilichofanyika mara wakati wa  kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo.
Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  ( wapili kutoka kulia  ) akiwasalimu baadhi ya wafanyanyakazi na viongozi wa Kampuni ya MMC  ya uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae  wakati wa  ziara  ya kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo  akifuatiwa na  Mkuu wa wilaya ya Mvomero ,Mohamed Utaly.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad