HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 12, 2018

Arsenal na Chelsea kutua dimbani kesho UEFA Europa League

Kocha Maurizio Sarri na Unai Emery wako katika nafasi nzuri kwenye makundi yao na wala hawana presha ya matokeo kuelekea mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi hivyo tutarajie upangaji wao wa vikosi kuwapumzisha wachezaji nyota. Kikosi cha Sarri (Chelsea) licha ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Manchester City wikendi iliyopita tayari wameshajihakikishia kumaliza wakiwa vinara wa kundi L katika ligi ya Europa.

Kocha huyo muitalia anatarajia kuwapatia nafasi wachezaji ambao huwa hawapati namba kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Na mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Eden Hazard amesema wanahitaji kuachana na ushindi wa lioupata dhidi ya Manchester City na kuangalia mechi zijazo. “Unahitaji kuangalia zaidi kile unachotakiwa kufanya. Sisi tunataka kushinda, tunafurahi tumeshinda mchezo uliopita na tunajiandaa na mchezo wa Alhamisi (dhidi ya MOL Vidi)

Kwa upande wa kocha wa Arsenal, Unai Emery yeye ana Vijana zaidi ya 10 walio chini ya umri wa miaka 20 na huenda akawatumia hao katika mchezo wao dhidi ya Qarabag huko nchini Azerbaijan.
Kutoka Bundesliga klabu ya RB Leipzig ambayo msimu uliopita ilicheza kwenye ligi ya mabingwa Ulaya, safari wanahitaji kushinda mchezo wao dhidi ya Rosenborg huku wakitegemea ndugu zao Red Bull Salzburg washinde jijini Glasgow dhidi ya Celtic.

Balaa lingine ni kwa klabu ya AC Milan ambao wanafunga safari hadi Ugiriki kuumana na Olympiacos, wakiruhusu kufungwa magoli 2 watakuwa mameaga mashindano. Michezo yote hii itaonyeshwa moja kwa moja kupitia StarTimes. MOL Vidi vs Chelsea saa 1:55 Usiku kupitia ST World Football, Arsenal vs Qarabag saa 5:00 Usiku kupitia World Football na Olympiacos vs AC Milan saa 5:00 Usiku kupitia ST Sports Premium. Chaneli zote hizo zinapatikana katika kifurushi cha MAMBO (Antenna) kwa Tsh 14,000 tu kwa mwezi na SMART (Dish) kwa TSh 21,000 kwa mwezi, ambapo katika msimu huu wa Siku kuu kila mteja atapata kifurushi cha juu zaidi kila anapolipia kifurushi chake kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad