HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 13, 2018

HUU NDIO UJUMBE WA DIAMOND PLATNUMZ KWA BASATA BAADA YA WIMBO WAO KUFUNGIWA



Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
WAKATI kukiwa na mjadala mkubwa katika medani ya tasnia ya burudani nchini baada ya wimbo wa Mwanza maarufu kama Nyegezi  uliombwa na wasanii wa lebo ya WCB kupitia mwanamuziki wake maarufu Nasseb Abdull’Diamonda’ na Raymond Mwakyusa a.k.a Rayvvany kuzuiliwa na Baraza la Sanaa Tanzania(Basata) Diamond amevunja ukimya.

Kupitia ukurasa wake Instagramu Diamond ameamua kutoa maelezo marefu ya kujitetea na kuelezea hatua kwa hatua hadi kilichosababisha wimbo huo kufungiwa.

Diamond kwenye ukurasa huo ameanza kwa kwa kusema hivi “Kwanza kabisa niwapongeze kwa kazi nzito na nzuri mnayoifanya....lakini pia niwape pole kwa changamoto mbalimbali mnazokutana nazo, maana najua ugumu mnaopitia katika kusimamia sanaa yetu nchini...

“Ujumbe wenu kuhusu kufungiwa wimbo wa #Mwanza almaarufu kama #NYEGEZI wakuu nimeupata ila tu kwabahati mbaya mtoto wenu niko Canada katika harakati za kutafta riziki ili kuendelea kulijenga Taifa na kuendelea kutangaza sanaa zetu, ila laiti ningelikuwa nchini ningekuja mara moja kama mnavyonijuaga pindi mniitapo basi hufika haraka bila ukaidi…
Tukiwa kama wasani ambao tumesajiliwa tuna kila haki ya kuheshimu na kutii baraza letu la BASATA pindi linapotoa tamko… kwasababu wao ndio wazazi na walezi wetu kwenye hii sanaa....na kwa kutambua kuwa sanaa ni kazi ya ubunifu na kwenye kubuni wakati mwingine kuna kuwa na usawa na wakati mwingine kutokuwa sawa.

“Ndio maana mliteuliwa ninyi wazee wetu maalum kwa ajili ya kuhakikisha wasanii wanapotoka nje ya mstari mnawarudisha ili tuwe na sanaa iliyo bora, tuzidi kufanikiwa, na kukua vyema na hata wasanii, mashabiki pamoja na Taifa kwa ujumla lijivunie na linufaike na sanaa.....
ila kwenye ufungiwaji huu nami nilikuwa nina ombi au pendekezo kwa baraza letu pendwa la BASATA,”amesema Diamond

Ameongeza kuwa “Licha ya kuwa ni kweli #NYEGEZI ni eneo na kituo cha mabasi kilichopo MWANZA, lakini pia ni vyema kama baraza letu pendwa la sanaa kutambua pia kuwa si  kila nyimbo ni kwajili ya watoto wadogo....Hivyo kusema isipigwe kwenye TV na Radio tumekubali, lakini iwe kwenye ule muda ambao Serikali uliuweka wa kuwa watoto wako macho, ila pale wanapolala, basi uruhusiwe ili walengwa wautazame.

“Pili kusema tuifute mitandaoni pia, naomba baraza letu pendwa litutazame pia na hapo.... kwasababu mtoto mdogo tunaemlenga kumlinda asiharibikiwe kimaadili hapa, sidhani kama mzazi wake anaweza kumruhusu akaperuzi bila mipaka mitandaoni maana kama kweli ana uwezo wa kufanya hivyo basi anauwezo wa kwenda kuangalia hata video za utupu, na vitu vingine ambayo wote tunafahamu ndio hatari na madhara zaidi kwa watoto,  kuliko hichi kinyimbo chetu cha #MWANZA NYEGEZI.”

Diamond ameendelea kufafanua kupitia ujumbe wake huo kwamba “ Wazee wetu, vijana wenu ama wasanii wenu sasa hivi tumefanikiwa kuingia kwenye masoko mbalimbali, hivyo si kila nyimbo ni kwajili ya soko la nyumbani Tanzania tu, mfano:Uganda kuna tamasha linaitwa NYEGE FESTIVAL....na kwa nafasi niliyonayo Uganda na kwa jinsi nyimbo hii ilivyovuma kwa kishindo kila kona ndani ya siku tatu tu Viewers 1.5+ Millions Youtube.

“Basi naamini kabisa mwakani lazima NYEGE FETIVAL waniite kutumbuiza...na kama mnavyofahamu bei zangu huwaga si chini dola za Marekani 70,000  kwa show
 sawa na Sh.milioni 160,300,000 .Kwa show moja tu ningeweza kuchangia pato la kodi si chini ya Sh.milioni 48.Hivyo naomba mlitazame na hapo Baraza letu pendwa,”amesema.

Pia Diamond ameongeza kuwa “Pia ikija upande wa kiuitumbwiza stejini naomba pia mlitazame zaidi...maana show zetu zote ni za usiku wa manane ambapo watoto wamelala majumbani Tunaowaimbia ni Watu wazima...
na hata #WasafiFestival2018 pia ifikapo saa 12 jioni ni wenye Umri wa zaidi ya miaka 18 tu....hivyo tutaowaimbia ni watu wazima tu

Pia amesema “Wazee wangu wa BASATA nilikuwa naomba muipe sikio tena nyimbo pale kwenye kipande cha Amber Rutty.. kwasababu ujumbe wangu pale ni kupingana na kile kitendo, na ndio maana nikasema "kananivuta ghetto nikapige Bunduki,... ila naogopa Centro michezo ya Amber Rutty" ...

“sasa hapo ubaya wake uko sehem gani...maana naamini kupitia mstari huo utakuwa ni kama kumbusho kwa kijana ama mtuyoyote kuwa "usidiriki kufanya, Utapelekwa jela..." sasa hapo wapi ubaya wake wazee wetu....

Amesisitiza kwa kueleza “Wazee wangu wa Basata ni siku tatu tu tangu kutoka kwa wimbo huu, lakini kika mwana Africa na hata asiekuwa  mwana Africa ashapajua Nyegezi Mwanza....na naamini kulikuwa na wengi pengine hawapajui lakini kupitia wimbo huu sasa wamepajua..na naamini wengi wanatamani hata wafike wapigepicha , wakapashangae kuwa kumbe #NYEGEZI kwenyewe ndio hapa....na hio ndio miongoni mwa faida ya kazi ya sanaa wazee wetu....
“Mie yangu yalikuwa ni hayo tu,  naamini kwa uelewa wenu na upendo wenu mlionao kwa sanaa na wasanii wenu, mtatusaidia kwa hayo maombi yetu vijana wenu...shukrani”.Huo ndio ujumbe wa Diamond Platnumz kwa Baraza la Sanaa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad