HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 13 November 2018

MAWAKILI WABISHANA KWA HOJA MAKAHAMANI KATIKA KESI INAYOWAKABILI VIGOGO WATATU WA KLABU YA SIMBA


Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema Novemba  26, 2018 itatoa uamuzi wa kama itapokea nyaraka za  taarifa ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda nyingine kama kielelezo cha ushahidi katika kesi 
ya utakatishaji  na kughushi dhidi ya viongozi watatu wa Klabu ya Simba ama la.

Hatua hiyo, imefikiwa leo Novemba 13, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas baada ya kuibuka mabishano ya kisheria ya  upande wa mashtaka na ule wa utetezi.

 Wakili wa Serikali Mwandamizi Shadrack Kimaro ameiomba  Mahakama hiyo isipokee nyaraka hizo kama kielelezo cha ushahidi huku Wakili wa utetezi uliokuwa ukiwakilishwa na jopo la mawakili likiongozwa na Wakili Wabeya Kung'e ukiiomba ukipinga isipokelewe.

Wakati Wakili Kimaro ameomba Mahakama ipokee nyaraka hizo ambazo zimetolewa mahakamani hapo na shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka,  Boaz Mbupila (45) kutoka Makao makuu ya Benki ya CRDB.

Kimaro amedai, Mbupila ndiye aliyezipeleka nyaraka hizo Takukuru
 ameeleza amezitoa benki na kuwa yeye ndiyo aliyezigonga muhuri na kuzisaini.

Alisisitiza kuwa nyaraka hizo zimetoka katika benki ya CRDB ambayo ni benki inayotambulika na ni miongoni mwaka benki hapa nchini ambayo inaheshimika,

Kimaro ameongeza kudai kuwa shahidi hiyo wa upande wa mashtaka alieleza mahakama kuwa nyaraka hizo zipo katika mfumo wa benki na utetezi ahawajaeleza ni kwa namna gani mfumo huo una matatizo.

Hivyo aliomba Mahakama kuona mapingamizi ya upande wa utetezi hayana mashiko, pia hawajaweza kufafanua hoja nzito ambayo inaweza kuizuia mahakama kupokea kielelezo hicho.

Kwa upande wa utetezi, Wakili Wabeya amedai Wakili Kimaro hajaelewa pingamizi lao wala hoja zao.

Amedai nyaraka za taarifa za kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda nyingine shahidi hakuweza kueleza na kufuata vigezo ambavyo vimewekwa kwani hakueleza kuwa yeye ndiye mhusika wa hizo nyaraka alichoeleza ni kuwa yeye aliziprinti na Kuzisaini na siye aliyeziingiza kwenye mfumo huo wa benki.

Wakili Wabeya aliendelea kudai kuwa shahifdi huyo wa upande wa mashtaka hakuweza kueleza hata mahakama kuwa taarifa hizo zilitunzwaje tunzwaje hadi yeye kuja kuziprinti na huo mfumo wakati  anaprinti alikuwa unafanya Kazi vipi.

Kutokana na mabishano makali ya pande zote mbili Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 26, mwaka huu kwa ajili ya uamuzi wa kielelezo hivyo.

Hata hivyo kesi hiyo itaendelea kusikiliza kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka Desemba 4 na 5, mwaka huu.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni  Rais wa Klabu hiyo,  Evans Aveva,  Makamu wa wake,  Geofrey Nyange na Mwenyekiti wa  Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad