HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 13 November 2018

MFUMO WA USAMBAZAJI MAJI WA BAGAMOYO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA KUBWA

Wataalamu wakiwa katika eneo la ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji Bagamoyo uliokamilika kwa asilimia kubwa na kufika katika tenko la Bagamoyo linalohifadhi maji lita 6 kwa siku.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wamesema  kazi ya   ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji Bagamoyo imekamilika kwa asilimia kubwa maji yamefunguliwa na kufika katika tenki la Bagamoyo. 

Kazi ya usafishaji wa mabomba inaendelea kwa ufanisi  na inatarajiwa kukamilika  leo chini ya usimamizi Mhandisi  Lydia Ndibalema Mkurugenzi wa miradi wa Dawasa

na utakapokamilika maji yataanza kwenda tenki la maji la Bagamoyo linalohifadhi Lita Milioni sita kwa siku.

Mradi huo wa  Uliojengwa kwa mkopo wa  masharti nafuu na unatarajiwa kukamilika rasmi mwezi Desemba mwaka huu na wananchi wa mji wa Bagamoyo watafanikiwa kupata maji.

 Zoezi hilo la kusafisha mabomba  mji wa Bagamoyo utaanza kupata maji  kwa wingi na  kwa msukumo mzuri kupitia mfumo wa zamani, Mkandarasi wa kujenga na kupanua mfumo mpya wa usambazaji maji anatarajiwa  kupatikana wakati wowote.

Mradi huo Oktoba 25 mwaka huu ulitembelewa na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu na kuahidi kufikia Desemba mwaka huu watakuwa wameshaanza kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni moja kati ya mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani.

Mradi huo unaotekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) ulianza rasmi mwezi Machi mwaka 2016 na utakamilika 2018.

Kazi ya mradi huo ipo chini ya mfumo unaohudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa ya kuhifadhi na kusambaza maji yenye ukubwa wa kuhifadhi lita Milioni 3.0 hadi 6.0.

Mbali na mradi wa matenki, kuna ujenzi wa vituo vinne vya kusukumia maji, ununuzi wa transfoma na ufungaji wa umeme wa msongo Mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji mitaani yatakayokuwa na urefu wa jumla ya Kilometa zipatazo 80.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad