HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 7 November 2018

BODI YA UTALII YAMTAKA MISS TANZANIA QUEEN ELIZABETH KUTANGAZA UTALII WA NCHI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imemkabidhi Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth baadhi ya vielelezo vya utalii ili akavitumie kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii kwa washiriki na watu kutoka mataifa mbalimbali. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Geofrey Tengeneza amesema kuwa Queen Elizabeth jukumu lake kubwa ni kushirikiana na bodi ya utalii katika kutangaza utalii wa ndani kwa maana ya kuvitangaza vivutio  vya utalii kwa watanzania na kuwahimiza kuvitembela vivutio vyetu hivyo.

 Amesema kuwa, mrembo huyu aliteuliwa kuwa Miss Domestic na tafanya kazi ya kutangaza vivutio vyote kwa kushirikiana na TTB na kwa kuzingatia hilo ndiyo maana leo  amefika ofisini kwao kwa ajili ya kuwaaga akielekea kuiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss World litakalofanyika nchini China . 

Mrembo wetu anatarajia kusafiri siku ya Ijumaa 9/11/2018 na atakuwa huko kwa mwezi mmoja mpaka siku ya kilele cha shindalo hilo litakalo fanyika tarehe 8/12/2018. 

Tengeneza amesema kwa niaba ya Bodi ya Utalii Tanzania wanapenda kuchukua  fursa hii kumtakia kila la heri na ushindi katika shindano hilo na pamoja ya kwamba yeye pia ni Miss 3 Domestic Tourism lakini kwa kutambua kuwa atakapokuwa huko China atakutana na washiriki wengine kutoka mataifa mbalimbali tumeona ni vema pia tumkabidhi baadhi ya vielelezo vya utalii ili akavitumie kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii kwa washiriki na watu kutoka mataifa mbalimbali. 

"Ni matumaini yetu makubwa kuwa ataifanya kazi hii vizuri na kwa uzalendo mkubwa, lakini tuna imani kubwa kuwa atafanya vizuri sana katika shindano hili na hasa ikizingatiwa kuwa Queen Elizabeth anayo rekodi nzuri sana katika mashindano ya urembo kwani mtakumbuka vizuri kuwa mbali ya kuwa Miss Tanzania anashikilia pia taji la mshindi wa kwanza la Miss World University Kundi la Afrika alilolinyakua huko Cambodia mwaka jana 2017,"amesema Tengeneza.

Kwa upande wa mnyane huyo Queen Elizabeth amesema kuwa ana uhakika taji la Miss World kwa mwaka huu linakuja nchini Tanzania kikubwa ni watanzania kumuombea na kumuunga mkono pindi atakapokuwa nchini China kwenye kipindi cha mwezi mmoja.

Queen Elizabeth amesema kuwa, vielelezo vya utalii alivyopewa atavitumia vizuri ikiwemo kutangaza lugha adhimu ya Kiswahili.

Tofauti na mashindano yaliyopita ya Miss Tanzania, mwaka huu washindi watanowalipewa hadhi na majukumu mengine ya kiutalii. Mshindi wa kwanza ambaye ndiye Miss Tanzania Bi Queen Elizabeth Mkune alipewa hadhi ya kuwa Miss Domestic Tourism na tafanya kazi hiyo chini ya uratibu wa TTB, mshindi mwnginemiongoni mwa hao watano amepewa hadhi ya kuwa Miss Ruaha National Park natafanya kazi chini ya uratibu wa TANAPA, mshindi mwingine alipewa hadhi ya kuwaMiss Ngorongoro, mwingine Miss Selous na mwingine Miss Nature and ecology.

 Kwa ujumla hawa wote watakuwa na majukumu ya kuyatangaza hayo maeneowaliyopewa. Kwa upande wa Bi Queen Elizabeth jukumu lake kubwa ni kushirikianana sisi katika kutangaza utalii wa ndani kwa maana ya kuvitangaza vivutio vyetu vyautalii kwa watanzania na kuwahimiza kuvitembela vivutio vyetu hivyo. Kazi hiii kamanilivyosema ataifanya kwa kushirikiana na sisi.
 Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Geofrey Tengeneza akimvalisha shuka la kimasai kwa  Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth kama moja ya vielelezo vya utalii ili akavitumie kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii kwa washiriki na watu kutoka mataifa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad