HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 7, 2018

PRECISION AIR YATOA PUNGUZO LA BEI KUADHIMISHA JUBILEE YA MIAKA 25

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KUELEKEA miaka 25 toka kuanzishwa kwa Shirika la Ndege la Kitanzania  limezindua mfululizo wa nauli zenye punguzo kubwa ambalo litawawezesha wale wote ambao hawajawahi kutumia usafiri wa Ndege kupata fursa ya kufanya hivyo.

Shirika hilo ambalo lilianzishwa mwaka 1993 na Mtanzania  Michael Shirima, ni miongoni mwa mashirika machache barani Africa yaliyoweza kudumu kwenye biashara kwa miaka 25 mfululizo. 


Akizungumzia sherehe hizo Meneja Masoko na Mahusiano Hillary Mremi amesema, Precision Air inajivunia mafanikio waliyoyafikia kama kampuni ya Kitanzania na kwamba sherehe hizo si za Precision Air pekee bali za nchi nzima. 


“ Huu ni ushahidi ya kwamba Watanzania wanauwezo wakuanzisha na kusimamia biashara zao wenyewe kama tunavyoelezwa mara kwa mara na Raisi wetu Mpendwa, Dkt.John Joseph Pombe Magufuli, ya kwamba tunauwezo wa kufanikiwa kwa jambo lolote ikiwa tutajiamini na kufanya kazi kwa bidii. Precision Air ni kampuni ya kitanzania, inayomilikiwa na Watanzania ambayo imepata kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa na Wananchi pamoja na Serekali na kutokana na uungwaji mkono huo leo tunaona matunda yake kwa kusherehekea miaka 25 ya kutoa huduma.” amesema  Mremi



“katika kushereherekea miaka 25 ya kutoa huduma tunazindua mfululizo wa nauli zenye punguzo kubwa ambalo litawawezesha wale wote ambao hawajawahi kutumia usafiri wa Ndege kupata fursa ya kufanya hivyo, na kwa kuanzia tumewapa nafasi ya watu wenye safari kati ya Dar – Kilimanjaro nafasi ya kujaribu huduma zetu kwa nauli ya Sh.50,000 tu ikiwa ni pamoja na kodi zote. Ofa hii inapatika kupitia tovuti yetu pamoja na ofisi zetu za mauzo. Tunapenda kuwataarifu wateja wetu kujiandaa kwani muda wowote ofa hii itahusika katika maeneo wanayo safari.” Mremi amefafanua zaidi.

Shirika la Precision ilianzishwa  kama kampuni ya Ndege za kukodi, ikitumia Ndege aina ya Piper Aztec inayobeba abiria watano, Precision Air limeendelea kukua na kuwa moja ya hadithi za mafaniko nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Ikiwa na Ndege tisa (9) aina ya ATR Precision Air sasa inafanya safari zake kutokea Dar es Salaam kwenda Arusha,Bukoba,Kilimanjaro, Kahama,Mtwara, Mwanza, Tabora, Zanzibar,Seronera,Nairobi na Entebbe ikitoa huduma ya uhakika ya usafiri wa anga katika maeneo hayo.

Baadhi ya mafanikio ambayo Precision Air imeafanikiwa kuyatima katika kipindi cha miaka ya karibuni ni pamoja na : -

Desemba 2015 – Tuzo ya Tanzania Leadership Awards - Kampuni Bora Upande wa mashirika ya Ndege 
2013 – Tuzo za TASOTA Shirika Bora la Ndege Tanznaia mwaka.
Februari 2012 – Aviation News Portal- Tuzo ya Shirika Bora la Mwaka Afrika- Tuzo ya shaba.
Desemba 2011 – Precision Air,ilikua shirika la kwanza la Ndege kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam.
Februari 2011 - Precision Air, izindua karakana ya kisasa yenye thamani ya Dola milioni 5.
2011 – Tuzo za TASOTA - Shirka Bora la Ndege Tanzania 
2010 – Tuzo za AFRAA –Shirika bora la safari za kikanda.
Oktoba 2009 – TCAA iliipatia Precision Air leseni ya kujihudumia yenyewe. 
2008 – Tuzo ya Mkurugenzi anayeheshimika Tanzania.
2007 – Tuzo ya Shirika linalo heshimika Tanzania.
2006 – Tuzo Za Tasota- Shirika bora la Ndege Tanzania.
Machi 2006 – Precision Air, ilikua shirika la tatu barani Africa kuanza kutumia mfumo wa tiketi za kieltroniki. 
Septemba 2006 – Ilipata cheti cha usalama cha IATA ikiwa ni shirika la kwanza Tanzania na la sita barani Africa. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad