HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 10, 2018

WAWEKEZAJI KATIKA RANCHI ZA TAIFA WATAKIWA KUSAINI MIKATABA MIPYA-NARCO

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
WAWEKEZAJI wa vitalu vya ufugaji katika ranchi ya taifa watakiwa kusaini mikataba mipya kwaajili ya kuendelea na ufugaji wa kibiashara katika ranchi za taifa hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) Philemon Wambura wakati wa kusaini mikataba mipya ya uwekezaji katika lanchi ya taifa jijini Dar es Salaam leo.

Wambura amesema kuwa mikataba hiyo mipya itaanza kutumika mara moja hivyo mwekezaji ambaye atakuwa hajasaini mkataba  mpya atahesabika kuwa hana nia tena ya kuendelea na uwekezaji kaika ranchi za taifa.

"Mikataba mipya itaanza kutumika mara moja hivyo mwekezaji ambaye atakuwa hajasaini mkataba  huu mpya atahesabika kuwa hana nia tena ya kuendelea na uwekezaji katika ranchi za taifa na hivyo ataondolewa". amesema Wambura

Amesema kuwa utaratibu wa kuwaondoa wawekezaji ambao hawana mikataba mipya katika ranchi za taifa utaanza kutekelezwa mara moja.

 Kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) iliingia mkataba na wawekezaji kwenye vitalu katika ranchi za taifa na wafugaji wadogo toka 2007 kwa nia ya kuwawezesha wafugaji wa asili kufuga kibiashara.

Hivyo kampuni hiyo imefanya tathimini ya uwekezaji kwa miaka kumi na kubaini kuwa baadhi ya vifungu vya mkataba havina tija kwa kampuni na uwekezaji.
  Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO), Philemon Wambura akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusaini mikataba mipya ya wawekezaji katika ranchi za taifa hapa nchini, kushoto ni Kaimu meneja wa fedha Ranchi za Taifa (NARCO) Nesta Kuza na kulia ni wakili wa kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) Alfred Shanyanga.
 Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) Philemon Wambura akisaini mikataba mipya ya uwekezaji katika ranchi za taifa jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu meneja wa fedha Ranchi za Taifa (NARCO) Nesta Kuza na kulia ni wakili wa kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) Alfred Shanyanga.
 Baadhi ya wawekezaji wakimsikiliza Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) Philemon Wambura mara baada ya kusaini mikataba mipya ya uwekezaji katika ranchi za taifa.
Baadhi ya wawekezaji wakisaini mikataba mipya ya uwekezaji katika ranchi za taifa. Mikataba hiyo imesainiwa leo Oktoba 10 ambapo ni mwisho wa kusaini mikataba hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad