HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 10 October 2018

TESEA KUNUFAISHA WANAFUNZI, WALIMU NCHINI ILI KULETA CHACHU YA ELIMU BORA

Na Khadija Seif Globu ya Jamii

MTANDAO wenye vifaa saidizi vya elimu umezinduliwa rasmi jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau wa elimu ,walimu na waandishi wa habari nchini.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwanzilishi wa Taasi isiyo ya kiserikali yenye mtandao wa kielimu nchini  (TESEA )Abdul Mambokileo amefafanua lengo la kuanzishwa kwa mtandao huo  unawataka wadau pamoja na walimu kuutumia kikamilifu kupata kuelewa baadhi ya mambo yanayohusu elimu ikiwemo maswali yatakua waongoza kuwafundisha wanafunzi na kufaulu .

Hata hivyo amesema  kumekuwepo na changamoto nyingi katika sekta ya elimu ukiachilia mbali suala la majengo,madawati pamoja na chakula zipo changamoto  ambazo kusababisha wanafunzi pamoja na walimu kukosa nyenzo za kujifunzia.

Mambokileo amefafanua aliiona fursa hiyo  na kuanzisha huduma ili kuipa kipaumbele elimu kwani msingi wa maisha mazuri ni pamoja kuwa na elimu ambayo itakuwezesha kupanga na kuendesha biashara,maisha huku ukiwa na ujuzi ambao unasaidiwa na elimu hata kama ni ya shule ya msingi .

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Taifa wa Shule binafsi Charle Ela  amepongeza juhudi hizo zinazofanywa na TESEA ambazo ipo kwa ajili ya kufanya mapinduzi ya kielimu na kusaidia Serikali kupunguza fedha kwenye kuwekeza katika sekta ya elimu.

Aidha,Totela amewapa ushauri walimu kuangalia upya swala la mafunzo ya vitendo ili kuboresha elimu bora kwani wanafunzi wengi wamekua wakijifunza zaidi kwa nadharia na kupeleka kudumaza akili zao.

Hivyo basi mtandao huo utawawezesha kujifunza zaidi kwani kuna silabasi ambazo zimewekwa pamoja na maswali mbalimbali na kuwataka wadau wengine kuleta mabadiliko na mapinduzi katika kuboresha elimu bora nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasi hiyo ya  elimu isiyo ya kiserikali (TESEA) amepongeza wadau,walimu kufanikisha kuzinduliwa kwa mtandao huo na kuomba waingie na kupakua kwa kuandika WWW.TESEA.COM .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad