HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 10, 2018

ASILIMIA 86 YA WANAWAKE NA ASILIMIA 100 YA WANAUME WA MKOA WA SHINYANGA WASEMA UMASIKINI NDIO SABABU KUBWA YA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

Asilimia 86 ya Wanawake na Asilimia 100 ya Wanaume mkoani Shinyanga wanasema kuwa umaskini wa familia ndio chanzo kikubwa cha mimba na ndoa za utotoni.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Shirika la Save The Children Bi. Neema Bwaira alipokuwa akitoa mada katika Mdahalo wa Kitaifa unaoendelea jijini Dar es Salaam kuhusu namana bora ya kupambana na ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni.

Bi Neema ameongeza kuwa waliamua kufanya utafiti huu mdogo ili kupata kujua uelewa wa jamii ya mkoa wa Shinyanga katika suala la mimba na ndoa za utotoni.

Ameongeza kuwa utafiti huo umefanyika katika Wilaya za Kishapu, Kahama na Shinyanga Mjini ambapo umebaini  kuwa jamii bado haina uelewa kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni na bado vitendo hivi vimekumbatiwa kwenye mwamvuli wa mila na desturi.

“Kwa mujibu wa utafiti huu mdogo tulioufanya tumebaini kuwa umasikini na uelewa mdogo wa jamii kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni” alisisitiza Bi. Neema.

Bi Neema ameeleza kuwa Asilimia 11 ya wavulana na  Asilimia 9 ya wasichana  wanaamini kjuwa ni haki kwa mwanaume kumpiga mke wake na wanaamini kuwa mke anapomkosea mume ana haki ya kukubali kupigwa na mume na anakubaliana na hilo  ili kuifanya familia iendelee kukaa pamoja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mdahalo huo na Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na watoto Dkt. John Jingu amesema kwa upande wa Serikali wanaendelea na mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa Wanawake na Watoto na wataendelea kushirikiana na wadau katika mapambano hayo.

“Kama Serikali tunachukua hatua na kwasasa sio swala la umri tu ila ukimuoa au kumpa mimba mwanafunzi wako kwenye hatari kubwa” Alisisitiza Dkt. Jingu

Aidha mmoja wa Mzee wa mila kutoka Dodoma Chief Lazaro Masuma amesema kuwa kwa mkoa wa Dodoma kuna tabia ya wazazi kuchukua mahari ya awali ya mtoto akiwa bado anasoma na kumuachisha shule hata kabla ya kumaliza darasa la saba.

“Haya mambo haswa yanaanzia kwenye pombe nasisitiza Serikali, wadau na wananchi tuendelee kutoa elimu juu ya athari za ndoa za utotoni kwa watoto wetu” alisema Chief Lazaro.

Naye mmoja wa Ngariba Mstaafu Bi.Rahel Masagara amesema kuwa wazazi wengi wamekuwa chanzo cha watoto kuingia katika tatizo la mimba na ndoa za utotoni kwani wanaume wengi wamekuwa wakiziacha familia zao na kuoa wanawake wengine ambapo watoto wanabaki hawana muongozo sahihi wa maisha.

“ Wababa tutulie na wake na familia zenu ili kuwapa malezi bora watoto wetu hasa wa kike kwa manufuaa yao, yetu na ya taifa “ alisisitiza Bi. Rahel

Wadau wa Maendeleo na Ustawi wa Mtoto wa kike wanaendelea na Mdahalo wa kitaifa unaojadili namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Mdahalo ambaye pia ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na watoto Dkt. John Jingu (kulia) akiongoza Mdahalo wa kitaifa unaojadili namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto Bi Mwajuma Mwagwiza na kushoto ni Muongozaji wa Mdahalo kutoka Shirika la UNFPA Zanzibar Bi. Amina Kheri .
  Mwakilishi wa Shirika la Save The Children Bi. Neema Bwaira  akitoa mada katika Mdahalo wa kitaifa unaojadili namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.
 Mzee wa Mila kutoka Dodoma Chief Lazaro Masuma akitoa ushuhuda katika eneo analotoka kuhusu suala la ukeketaji, Mimba na Ndoa za Utotoni katika Mdahalo wa kitaifa unajadilia namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa Ngariba Mstaafu Bi.Rahel Masagara akitoa ushuhuda akisisitiza wazazi kutimiza wajibu na majukumyu yao kwa watoto hasa wa kike kuhusu suala la ukeketaji, Mimba na Ndoa za Utotoni katika Mdahalo wa kitaifa unaojadili namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Maendeleo na Ustawi wa mtoto nchini wakifuatilia Mdahalo wa kitaifa unaojadili namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad