HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 19 October 2018

WASHINDI WATATU WAIBUKA KATIKA DROO YA WEKA DAU NA USHINDE

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
Kampuni ya kubashiri michezo nchini M BET ambayo imechezesha droo ya perfect 12 ambayo imetoa washindi zaidi ya 15.

Akizungumza na waandishi habari wa kutambulisha washindi hao Meneja Masoko wa M Bet Allen Mushi ameeleza Kasi ya washindi ambao wanaendelea kuweka ubashiri wao  na kujishindia pesa taslimu shilingi milioni 150.

Aidha,Mushi amewaambia washiriki kuwa perfect 12 ni droo mpya ambayo jackpot hiyo ni ya kila siku na dau linabadilika na kwa mshindi ambae hatopatikana kwa siku M BET itaongeza dau hilo kwa siku inayofata kwa watu watakaopatia ubashiri wa mechi husika. 

 Mushi  ametangaza washindi  watatu ambao wameweza kujishindia pesa na kwa sasa pesa zao zimeweza kuingia Kwenye akaunti zao kwa usalama zaidi.

Amesema mchezo wa kubashiri na M BET imebadilisha maisha ya wengi ambao pesa wanazozipata zimekua zikiendesha maisha yao binafsi na hata wengine kusomesha familia,kufungua biashara pamoja na kutimiza baadhi ya mahitaj muhimu katika jamii inayowazunguka.

Akitoa ushuhuda huo mshindi kutoka Mkoa wa Iringa katika wilaya ya Mafinga Meshack Ngole ambae ni Mjasiriamali  ameeleza mapokeo ya ushindi huo na pesa atapanua biashara yake ili kujikwamua kiuchumi kwani vijana wengi wamekua wakijiingiza Kwenye vitendo viovu kutokana na kukosa ajira .

Aidha, Ngole amewatoa hofu washiriki wanaobashiri na M BET kuwa hakuna ambae anapangwa au kutengenezwa uongo ili aonekane mshindi kama baadhi ya watu wanavosema na amewashauri waendelee kubashiri.
Meneja masoko wa  kampuni ya M bet  Allen Mushi (wa kwanza kulia) akiwa na washindi watatu wa perfect 12 wakati wakitoa ushuhuda wa ushindi huo mnono wa millioni 150 kwa kila mmoja

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad