HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 12 October 2018

WAFANYAKAZI BENKI YA TIB CORPORATE WAMTEMBELEA MKURUGENZI MSD KUSHEHEREKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

WAFANYAKAZI wa benki ya TIB Corporate  wamtembelea Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa jijini Dar es Saaam leo.

Uamuzi wa wafanyakazi wa benki hiyo kwenda MSD nimwendelezo wa kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja kwa namna ya kutembelea wateja wao kwaajili ya kutoa shukurani kwa wateja.

Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa amewashukuru benki hiyo kwani wamefanya kitu cha tofauti pia amewatia moyo kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na kujituma.
Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa akizungumza na wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate mara baada ya kumtembelea ofisini kwake ikiwa kushehereka wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika Oktoba kila mwaka. Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) mara baada ya kumtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD)  mara baada ya kumtembelea  ofisini kwake.
 Wafanyakazi wa bohari ya Dawa (MSD) wakimsikiliza mfanyakazi wa benki ya TIB Corporate hayupo pichani jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD)  mwenye tisheti ya bluu leo mara baada ya kutembelewa na wafanyakazi hao ofisini kwake.
Mfanyakazi wa benki ya TIB Corporate akiangalia boksi la dawa mara baada ya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa kuwaonesha jinsi bohari hiyo ilivyo.
Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa  akiwaonesha baadhi ya maboksi ya dawa wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakiwa  kutembelewa na wafanyakazi hao  jijini Dar es Salaam na kuangalia mteja wao anavyofanya kazi.


Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakitembelea bohari ya dawa (MSD)mara baada ya mazungumzo na mkurugenzi mkuu wa bohari ya dawa jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika Oktoba kila mwaka.
Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakipata maelezo mara baada ya kufika kitengo cha usafirishaji dawa.

Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate akiangalia jinsi bohari ya dawa (MSD) wanavyofanya kazi zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad