HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 12 October 2018

MWILI WA PANCHO LATINO WAAGWA LEO JIJINI DAR, KUSAFIRISHWA KWENDA GAIRO KWA MAZISHI

 Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MWILI wa aliyekuwa mtayarishaji wa muziki nchini Joshua Saimon Magawa maarufu kama Pancho Latino umeagwa katika viwanja vya Lugalo na kusafirishwa kuelekea Gairo kwa ajili ya mazishi. 

Msemaji wa familia amesema kuwa mpendwa wao alizaliwa 11/5/1988 na  alifariki dunia 9/10 mwaka huu akiwa anaogelea kisiwani Mbudya jijini Dar es salaam, Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa anajihusisha na shughuli za utayarishaji wa muziki  (Producer)
Kwa upande wake rapa maarufu Mabeste ambaye nyimbo zake zilifanywa na marehemu ameshindwa kabisa kujizuia kutokana na ukaribu hasa msaada wa marehemu Pancho  katika muziki wake na  amewahimiza wasanii kupendana kama marehemu ambaye alikuwa ni upendo kwa wenzake.

Wasanii na watayarishaji wa muziki wamejitokeza kumuaga Pancho Latino huku wakihimiza upendo baina yao katika maisha yao hapa duniani.
Marehemu ametengeneza hits kadhaa zikiwemo closer ya Vanessa Mdee na Dar es salaam stand up ya Chid benz na anatarajiwa kumpumzishwa kesho huko Gairo(Msingisi)  mjini Morogoro.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe amina.
 Sehemu ya Waombolezaji wakipita kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mtayarishaji wa muziki nchini Joshua Saimon Magawa maarufu kama Pancho Latino, aliyefariki Dunia hivi karibuni.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Mabeste akiwa ni menye huzuni sana wakati wa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa mtayarishaji wa muziki nchini Joshua Saimon Magawa maarufu kama Pancho Latino.
 Sehemu ya Waombolezaji

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad