HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 12 October 2018

WANANCHI WALINDE VYANZO VYA MAJI - PROFESA MBARAWA

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profesa Makame Mbarawa amewataka wananchi wanaoishi pembezoni mwa vyanzo vya maji kuvilinda ili viwafaidishe.

Mbarawa ameyasema hayo baada ya kutembelea mradi wa maji wa Mtoni unaozalisha maji Lita Milioni tisa kwa siku.

Akizungumza baada ya kumaliza kukagua chanzo cha Maji cha Mto Kizinga, Profesa Mbarawa amesema kuwa wananchi wanatakiwa kulinda vyanzo vya maji ili kuweza kupafa maji ya uhakika.

Mbarawa amesema mradi wa maji wa mtoni una uwezo wa kutoa maji Lita Milioni tisa kwa siku ambayo inachagiza katika uzalishaji wa maji  katika Mkoa wa Dar es Salaam

Amesema, kwa pamoja wananchi wanatakiwa washirikiane kulinda mazingira kwani Maji ni uhai na watakapoharibu vyanzo  watasababisha ukosefu wa maji ya kutosha.

"Kwa pamoja inabidi tushirikiane na wananchi kuwapa elimu ya umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji, watakapoviharibu vyanzo hivi watasababisha maji kupungua na muda mwingine kuharibu kabisa vyanzo," amesema Profeaa.

Mbali  na hilo, Mbarawa ameeleza kuwa lengo lingine ambalo wameshakubaliana ni kupanda miti pembezoni mwa vyanzo vyote vya maji ili kuvilinda.

Meneja wa Mradi wa Mtoni Deusdedit Rwegasira amesema kuwa chanzo cha maji cha mto Mzinga umeweza kuwasaidia wananchi wa Mtoni Kijichi, Mtoni, Kurasini na baadhi mengine ya Chang'ombe na ndani ya miaka mitatu hakijawahi kupungua kwenye uzalishaji.

Mkoa wa Dar es salaam una mahitaji ya maji Lita Milioni 544 kwa siku ila katika mtambo wa Ruvu Juu na Ruvu Chini kwa pamoja unazalisha Lita 504 kwa siku.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akiwa anatembelea mradi wa maji wa mtoni unaozalisha maji Lita Milioni tisa kwa siku unaowafaidisha wananchi wa Mtoni, Mtoni Kijichi, Kwa Azizi Ali, Kurasini na baadhi ya maneo ya Chang'ombe.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akiwa anatembelea mradi wa maji wa mtoni unaozalisha maji Lita Milioni tisa kwa siku unaowafaidisha wananchi wa Mtoni, Mtoni Kijichi, Kwa Azizi Ali, Kurasini na baadhi ya maneo ya Chang'ombe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad