HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 25, 2018

USAILI BONGO STAR SEARCH KUFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO

BAADA  ya kukamilika kwa Usaili wa Shindano la Bongo Star Search katika mikoa minne ya Tanzania bara ikijumuisha Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam sasa usaili huo utaendelea kupitia mitandao ya kijamii hasa Instagram na Facebook.
Usaili huo wa mtandaoni unatarajiwa kudumu kwa muda wa wiki tatu kuanzia leo Oktoba 25 ambapo mshindi ataingia kambini  kwa mafunzo kutoka kwa walimu na hatua ya mchujo itafuata.

Akizungumza na vyombo vya habari jaji mkuu wa mashindano hayo na Mkurugenzi Mkuu wa Benchmark Rita Poulsen amesema kuwa; “Ni nafasi ya kipekee kabisa kwa watanzania kushiriki na kupata nafasi ya kujiunga na BSS msimu wa 9, kwa sababu kama mlivyoona kwa mwaka huu tumeenda mikoa michache zaidi ni kutokana na sababu ambazo zimekuwa nje ya uwezo wetu, ila kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya BSS tunatoa nafasi ya ushiriki kupitia Mitandao ya kijamii” amesema MadamRita.

Aidha amesema kuwa “Kushiriki ni rahisi sana unachotakiwa kufanya ni kurekodi video ukiwa unaimba, video isiyozidi dakika moja ama sekunde sitini kisha post katika mtandao wa Instagram au facebook kwenye akaunti yako tag akaunti za @startimestz na @bongostarsearch na uambatanishe na hashtag #BSSOnlineAudition ili video yako iweze kutufikia na kufanyiwa usaili na majaji”. Aliongezea Madam Rita.

Hatua ya mchujo inatarajiwa kuanza katikati ya mwezi wa kumi na moja baada ya usaili wa mtandaoni kukamilika. Shindano la BSS msimu wa tisa linaendelea kurushwa na kituo cha StarTimes Swahili katika king’amuzi cha StarTimes kila siku saa tatu Usiku. Chaneli inayorusha mashindano hayo   ipo katika kifurushi nafuu kabisa cha Nyota ambacho kinagharimu Tsh 8000 tu kwa watumiaji wa dikoda za Antenna na Tsh 11,000 kwa watumiaji wa dikoda za Dishi kote nchini.

Pia imeelezwa kuwa mshindi wa Usaili wa mtandaoni anatarajiwa kutangazwa tarehe 18 Novemba mwaka huu na atasafirishwa kutoka popote pale nchini hadi Dar es Salaam kujiunga kambini na washiriki wengine 16 ambao tayari wameshapatikana katika Usaili wa mikoa 4 ya Tanzania bara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad