HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 28, 2018

SWEDY MKWABI AZINDUA KAMPENI ZA UENYEKITI WA KLABU YA SIMBA

Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Klabu ya Simba SwedyMkwabi akielezea mikakati yake ndani ya Simba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi wa klabu hiyo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 
 MGOMBEA wa nafasi ya uenyekiti wa Klabu ya Simba Swedy Mkwabi ameweka wazi mikakati yake iwapo atapewa ridhaa na wananchama wa Klabu hiyo kuiongoza kwa kipindi kijacho. 

 Mkwabi amezindua kampeni zake leo Jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na wanachama wa klabu ya Simba kutoka matawi mbalimbali. 

 Akizungumza wakati wa kuzindua kampeni zake, Mkwambi amesema kuwa atahakikisha anasimamia vizuri mfumo wa mabadiliko wa uendeshaji wa klabu ya Simba kulingana na katiba mpya ya toleo la mwaka 2018 kama ilivyopitishwa na wanachama. 

 Mkwabi amesema, suala lingine ni kuona klabu ya Simba inakuwa na vyanzo vya mapato endelevu na vya uhakika ikiwemo na kufanya vizuri katika mashindano ya kitaifa  a kimataifa ili litawezekana kwa kusimamia kwa weledi na kuheshimu taaluma ya walimu na benchi la ufundi. 

 "Katika kuhakikisha maslahi ya wanachama wa Simba yanalindwa vizuri kwa kushirikiana na muwekezaji mkuu wa Simba ni kuondoa makundi ya wanachama na kutengeneza umoja wenye nguvu na kufuata, kuheshimu katiba ya Simba,"amesema Mkwabi.

 Ameweka wazi mkakati mwingine ni kuwa na ushirkiano wa karibu kati ya uongozi wa makao makuu na uongozi wa matawi, Wilaya na Mkoa ili kuleta ufanisi na umoja ndani ya Klabu ya Simba, Kuhakikisha mila na desturi na utamaduni wa klabu hiyo inadumishwa na kuendelezwa. 

 Mkwabi amezindua kampeni yake leo na kuanzia Oktoba 29 atakutana na viongozi wengine wa matawi wa Wilaya ya Temeke ili kunadi sera zake na amesema kuwa akipewa nafasi ya kuwa mwenyekiti atatumia uzoefu wake wa uongozi wa mpira wa miguu na kushirikiana na viongozi wenzake pamoja na mwekezaji ya klabu hiyo ili kutengeneza dira ya maendeleo ya michezo.

 "Nitahakikisha Simba inakuwa klabu bora sio tu Tanzania bali Afrika kwa ujumla, nitahakikisha tunakuwa na miundo mbinu ya michezo kama viwanja vya michezo, hostel, shule ya michezo kwa vijana na soka la wanawake," amesema Mkwabi.

Katika uongozi wake, Mkwabi ni Mwenyekiti wa Mpira wa Miguu wilaya ya Tanga kuanzia 2013 hadi sasa hivi ila amewahi kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji  wa klabu ya Simba kuanzia mwaka 2010 hadi 2014 na mwenyekiti wa kamati ya mashindano mwaka 2012 hadi 2014 na iwapo atachaguliwa atakuwa moja kwa moja anapata nafasi ya kuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya Simba. 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad