HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 27 October 2018

WATANZANIA TUENDELEZE UTAMADUNI WETU-MAJALIWA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwadhama  Polycarp Kardinali Pengo wakati alipowasili kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salam kushiriki katika  Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania kwa Jamii ya Watu wa Mkoa wa Lindi, Oktoba 26, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na Mwadhama  Polycarp Kardinali Pengo wakati alipowasili kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salam kushiriki katika  Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania kwa Jamii ya Watu wa Mkoa wa Lindi, Oktoba 26, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amekaa katika mazingira ya asili wakati aliposhiriki katika  Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania kwa Jamii ya Watu wa Mkoa wa Lindi lililofanyika  kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam, Oktoba 26, 2018
 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vyakaula vya asili wakati aliposhiriki katika Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania  kwa Jamii ya Watu wa Mkoa wa Lindi  lililofanyika kwenye kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam, Oktoba 26, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda mti wa asili wakati aliposhiriki katika Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania  kwa Jamii ya Watu wa Mkoa wa Lindi  lililofanyika kwenye kijiiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam, Oktoba 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuuheshimu na kuuendeleza utamaduni ambao ndio urithi wao ili kulifanya Taifa liendelee kuwa hai.

Amesema suala la kuuenzi utamadini ni jambo zuri ambalo linatoa fursa kwa watu wengine hususan wa mataifa ya nje kuja kujifunza historia ya Watanzania na maisha yao.

Waziri Mkuu aliyasema yao jana jioni (Ijumaa, Oktoba 26, 2018) alipotembelea shughuli za tamasha la utamadini wa Mtanzania kwa jamii ya watu wa Lindi.

Katika tamasha hilo linalofanyika kwenye Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania waendelee kuupenda utamaduni wao.

“Nimefurahi kuona nyumba zikiwa na zana mbalimbali za kitamaduni ambazo zilikuwa zikitumiwa na wazee wetu pamoja na namba ya utayarishaji wa vyakula vyetu vya asili.”

“Sikutarajia kuona haya ninayoyaona, nawashukuru wote walioshiriki katika kandaa tamasha hili pamoja na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Kijiji cha Makumbusho.”

Waziri Mkuu alisema tamasha hilo ambalo limewakutanisha Wanalindi kutoka katika wilaya mbalimbali linatoa fursa ya wao kujadili maendeleo ya mkoa wao na Taifa kwa ujumla.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwaomba wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda katika Kijiji cha Makumbusho kwa ajili ya kujifunza historia ya mkoa wa Lindi pamoja na fursa zilizoko.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema mkoa umetumia tamasha hilo kutoa ujumbe kwa umma kuhusu vivutio mbalimbali walivyonavyo pamoja na fursa za uwekezaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad