HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 1, 2018

SONGAS yatoa rambirambi ya milioni 50 kwa wafiwa kufuatia tukio la ajali la MV Nyerere

Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Issack Kamwelwe (wa pili kushoto) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 50 kutoka kwa Meneja wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Uzalishaji Umeme nchini Songas Limited, Bi. Agatha Keenja (wa pili kulia) ikiwa ni kama rambirambi kwa ajili ya kusaidia shughuli za kuhudumia wahanga wa ajali pamoja na mkono wa pole kwa wafiwa kufuatia tukio la ajali la MV Nyerere. Hafla hiyo imefanyika  mwishoni mwa juma visiwani Ukerewe jijini Mwanza. Wengine katika picha kulia ni Meneja Miundombinu wa kampuni ya Uzalishaji Umeme ya Songas Limited, Bw. Goronga Kasaka.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (katikati) na wadau wa SONGAS mara baada ya makabidhiano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa juma visiwani Ukerewe jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad