HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 1, 2018

DAWASA WAANZA UJENZI WA BOMBA KUBWA LA MAJI BANDARINI

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) wameendelea kuboresha huduma ya maji sehemu mbalimbali ikiwemo kuongeza maji ya kutosha katika bandari ya Dar es Salaam.

Mkakati huo umeanza kutekelezwa rasmi  na Mkoa wa Dawasa Ilala kwa kuanza zoezi maalum la kuunga Bomba kubwa la kipenyo nane ili  kupeleka Huduma ya maji ya kutosha Bandarini.

Meneja wa mkoa Ilala Judith Singinika  amesema kuwa zoezi linatekelezwa kulingana na agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profesa Makame Mbarawa  alilolitoa alipotembelea mamlaka hiyo ya Bandari.

Amesema kuwa, kukamilika kwa zoezi la kuunga bomba hilo kutaongeza wingi wa maji katika bandari hiyo ya Dar es salaam na kuhakikisha kuwa mahitaji ya huduma ya maji kwenye eneo lote la Bandari yanafikiwa. 

Aidha kazi hii itawezesha pia meli zote za abiria na mizigo zinazotia nanga katika bandari hii kibwa kuliko zote nchini zinapata maji safi na kukidhi mahitaji.

Hapo awali, Bandari walikuwa wananunua maboza kutoka nje kwa ajili ya matumizi ya meli zinazotia nanga na Profesa Mbarawa alipiga marufuku na kuwataka watumie maji ya Dawasa kwa usalama zaidj.

Kazi hii ni utekelezaji wa  agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profes Makame Mbarawa alilolitoa tarehe 30/7/2018 wakati wa ziara ya ya kutambua Wateja wakubwa wa maji Dar es salaam.
Ujenzi wa kuunga bomba kubwa la maji lenye kipenyo nane ili  kupeleka Huduma ya maji ya kutosha Bandarini ukiendelea kufuatia agizo la Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profes Makame Mbarawa alilolitoa tarehe 30/7/2018 wakati wa ziara ya ya kutambua Wateja wakubwa wa maji Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad