HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 13 October 2018

PROFESA MBARAWA AAGIZA DAWASA WAANZE KUVITUMIA VISIMA VYA KIMBIJI MPERA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa ametoa maagizo kwa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka DAWASA kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi kwenye visima vilivyokamilika.

Amesema hayo baada ya kutembelea visima vilivyopo mpiji vinavyojengwa na Kampuni ya Serengeti katika mradi ulioanza 2014 utakaowezesha upatikanaji wa maji katika maeneo mengi ya Jijini Dar es salaam na Pwani.

Akizungumza baada ya kumaliza kuvikagua visima hivyo, Mbarawa amesema kuwa visima vilivyokuwa vimekamilika vianze kujengwa matanki ili wananchi waanze kupata maji Safi na salama.

Mbarawa amesema, "DAWASA msisubiri mkabidhiwe visima vyote kutoka kwa mkandarasi kwa sasa mnatakiwa mjenge matanki kwa ajili ya kuhifadhi maji na kuanza kuwahudumia wananchi,"

“Visima vya Kimbiji vipo tayari na hapa nimetembelea kisima ch M1, 2 na 5 na viwili hapo vimekamilika M1 kikitoa Lita 120,000 kwa saa na M5 Lita 100,000 kwa saa, ni hatua kubwa kwakuwa vimeshakamilika.”

Amesema, visima vya Kimbiji vimeshakamilika na viwili vya Mpiji vipo tayari na amewaagiza DAWASA kuhakikisha wanaanza kuvitumia ambapo awali walitaka kuvunja mkataba na Mkandarsi ila wakaacha suala hilo baada ya kuona watapata hasara ya kumtafuta mkandarasi mpya.

Kaimu Mkurugenzi wa  Miradi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka  DAWASA  Lidya Ndibalema  amesema kuwa watafuata kama maagizo yaWaziri aliyowapa ya kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi kutoka katika vile visima vilivyokuwa vimekamilika.

Amesema kuwa, wamekubaliana na Mkandarsi kuwa kila baada ya wiki mbili atawakabidhi kisima na wataanza kufanya dizaini mpya katika maeneo machache kuhakikisha wanaweka maji katika matankli ili kuwapelekea wananchi.

Mbali na hilo, Lyida amesema kuwa kama wataalamu walivyowaagiza watakuwa makini katika  masuala ya kimazingira na , watafanyia usanifu ili kuona chumvi isije  kuingia kwenye visima hivi.

Mradi huu wa Kimbiji na Mpera umegharimu takribani Bilioni 23 mpaka kukamilika kwake na lengo kuu la Serikali ni kuhakikihsha wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wanapata maji safi na salama na kwa Mkoa wa Dar es Saalaam Serikali imeweza kutumia Trilioni moja katika kipindi cha miaka mitatu kuboresha miundombinu ya maji kutoka Ruvu juu na Ruvu chini.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji  Profesa Makame Mbarawa akilezwa na Meneja wa mradi huo visima vya Mpijo na uwezo wake wa uzalishaji maji kwa saa.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akizungumza baada ya kukagua kukagua kisima cha M1 na M5 vilivyokuwa vimeshakamilika na kuagiza Mamlaka ya Maji Safi na Majo Taka DAWASA kuanza kuwahudumia wananchi wasisubiri mpaka kukabidhiwa visima vyote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad