HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 10 October 2018

MULTICHOICE YAZINDUA RASMI KITUO CHA MAFUNZO YA UANDAAJI FILAMU AFRIKA MASHARIKI

MultiChoice Africa imezindua rasmi kituo cha mafunzo ya uandaaji wa filamu  katika ukanda wa Afrika Mashariki . Sherehe za uzinduzi huo zimefanyika mjini Nairobi nchini Kenya katika makao makuu ya ofisi ya MultiChoice na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu pamoja na wawakilishi mbalimbali wa serikali  kutoka katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.

Baadhi ya viongozi wa serikali waliohudhuria katika uzinduzi huo mjinji Nairobi ni pamoja na Waziri wa Habari, Teknolojia na Mawasiliano Kenya, Mhe. Joe Mucheru, Katibu wa Wizara ya Habari na Mawasilano Kenya, Bi Fatma Hirsi, Mwenyekiti wa Baraza la Filamu nchini Kenya Chris Foot, Mwenyekiti wa bodi ya Filamu nchini Kenya Ezekiel Mutua, Kaimu Mkurugenzi Mkuu KBC Paul Jilani, wajumbe wa kamati ya bunge ya ICT kutoka Kenya akiwemo mheshimiwa John Kiarie huku Tanzania ikiwakilishwa kwa heshima kubwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza.

Akizingumza katika uzinduzi wa kituo hicho, Mkurugenzi wa MultiChoice Kanda ya Afrika Kaskazini.Maharage Chande alisema, “Tunaamini kuwa kuanzishwa kwa programu ya hii, kutatuhakikishia muendelezo wa utamaduni wetu waafrika wa kutoa hadithi zetu kwani huo umekuwa ni utamaduni wetu toka enzi na enzi. Ni katika utamaduni huu huu wa kiafrika, sasa tunapanda mbegu hii kwa vijana ili kuuendeleza utamaduni wetu huu adhimu kwa kizazi kipya na kijacho.

Tutambue kuwa uhai wa utamaduni huu unategemeana na kutengenezwa kwa fursa za kukuza weledi na umahiri katika uzalishaji wa kazi za kisanii zinazoakisi historia, mila, desturi na tamaduni zetu na kuhakikisha kuwa weledi na umahiri huo unaendelezwa. Naamini kuwa kwa kupitia programu hii ya MultiChoice Talent Factory ndoto yetu hii itatimia. “ alisema Maharage.

Vijana hawa 20 wa Afrika ya Mashariki , 4 kati yao kutoka Tanzania akiwemo Sara Kimario (25) Chalinze, Jamali Kishuli (23) Arusha, Wilson Nkya (24) Kigoma na Jane Moshi (25) Kilimanjaro wataanza rasmi programu hii ya mafunzo ya miezi 12 mapema mwezi huu  ambapo wataunganishwa na wataalamu waliobobea tasnia hii sambamba na mitaala iliyokidhi viwango vya kimataifa.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Teknolojia na Mawasilano nchini Kenya Mhe. Joe Mucheru, ameipongeza Kampuni ya MultiChoice kwa jitihada zake  hususani katika kuwekeza na  kuwainua na kukuza vipaji vya vijana wa kiafrika  kupitia  tasnia hii ya filamu. Alisema , “Nina imani  kuwa program hii itakuwa ni chachu kubwa katika kuleta mapinduzi kwenye tasnia ya filamu katika kanda yetu ya Afrika Mashariki. 

Ninaamini kupitia ujuzi watakaopatiwa vijana hawa watakuwa na uwezo wa kutengeneza kazi zenye ubora wa hali ya juu, wataweza kujiajiri wao wenyewe na pia watakuwa waalimu wa wenzao ambao wanavipaji katika tasnia hii. Ni matumaini yangu kuwa  darasa hili la 2018 litakuwa mfano wa kuigwa  kwa vizazi vijavyo ambao wangependa kuwa katika tasnia hii”, alisema Joe Mucheru.

“Kwa zaidi ya kipindi cha miaka 20 tumekuwa tukitumia nguvu nyingi katika kuongeza ubora na viwango vya kazi zetu bila mafanikio tuliyokuwa tukiyatarajia. Huu ni wakati sahihi kwetu kujiuliza swali hili, Ni njia gani sahihi inayotupasa kutumia ili kuongeza ubora katika kazi zetu”, Alisema Njoki Muhoho Mkurugenzi wa kituo cha mafunzo filamu cha MultiChoice Afrika ya Mashariki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad