HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 1, 2018

MKUTANO MKUBWA WA UONGOZI KUFANYIKA OKTOBA 19 JIJINI DAR


Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Mkutano Mkubwa wa Kwanza wa Uongozi utakaofanyika tarehe 19 Novemba 2018  jijini Dar es salaam 



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) kinatarajia kufanya Mkutano Mkubwa wa Kwanza wa Uongozi utakaofanyika tarehe 19 Novemba 2018 katika Hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es salaam ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye atawakilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama .

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)  Dkt Aggrey Mlimuka amesema l
engo kuu la mkutano huo ulioandaliwa na ATE kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (Confederation of Norwegian Enterprise, NHO) unalenga kuwaleta pamoja viongozi wa mashirika mbalimbali wakiwemo wanawake na wanaume ili kujadili namna ya kuongeza idadi ya viongozi wanawake katika nafasi za juu kabisa za uongozi.


Dkt Mlimuka amesema kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu ya ‘Uongozi wenye Ufanisi kwa Mazingira yanayobadilika Kibiashara’ na katika utafiti mbalimbali zimethibitisha kuwa taasisi na makampuni yaliyofanikiwa kuwa na wanawake katika nafasi za juu za uongozi yamepata matokeo chanya kama vile ongezeko la uzalishaji jambo ambalo Chama cha Waajiri wangependa kulifanikisha kwa wanachama wao na wasio wanachama pia katika kuunga mkono jitihada za kitaifa za kujenga Tanzania ya Viwanda ili kufikia Uchumi wa Kati ifikapo Mwaka 2025.





Aidha amesema kuwa, jitihada hizi zinaendana na juhudi ambazo zinafanywa na Chama cha Waajiri Tanzania na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) kwa kutoa mafunzo ya Mwanamke wa wakati Ujao (Female Future) yaliyozinduliwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshiwa Samia Hassan Suluhu mwaka 2016. Mpaka sasa jumla ya wanawake 66 wamepatiwa mafunzo haya ambapo awamu ya kwanza walikuwa 36 kwa mwaka 2016 na awamu ya pili walikuwa 30 kwa mwaka 2017. Sasa tupo kwenye awamu ya tatu ambapo wanawake 20 wanashiriki.

Dkt Malimuka ameelezea kuwa, Programu hiyo imefanikiwa kuandaa wanawake kwa ajili ya nafasi za juu za uongozi na kuwapa uwezo wa kuingia kwenye Bodi za Wakurugenzi na kushiriki katika kutoa maamuzi ambapo wanawake kadhaa waliohitimu tayari wamefanikiwa kupata nafasi za juu za uongozi na pia kuwa wajumbe kwenye bodi mbalimbali huku mchango wao ukionekana dhahiri.

Amewaomba wadau mbalimbali kushiriki katika Mkutano huu ili kujipambanua kama kampuni au taasisi zinazounga mkono jitihada za kuleta uongozi bora wenye kuleta maendeleo katika jamii nzima. Pia tumefungua milamgo kwa mashirika, makampuni na Taasisi mbalimbali ambazo zitapenda kujitangaza kupitia mkutano huu. 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad