HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 1, 2018

BENKI KUZITAMBUA HATI ZA HAKIMILIKI ZA KIMILA

Mratibu wa Mradi wa kuwezesha umilikishaji ardhi (LTSP) akitoa taarifa fupi ya mradi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na wafadhili wa mradi mjini Ifakara kabla ya kuanza ziara ya uwandani.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mathias Kabundugulu (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya (kulia) wakitia saini katika kitabu cha wageni kwenye ofisi ya kijiji cha mbuyuni ambapo pamoja na viongozi hawa, wafadhili wa mradi na wafanyakazi wa LTSP walishiriki katika ziara hii.
Afisa Ardhi mteule wa Wilaya ya Kilombero Syabumi Mwaipopo (alioyeshika karatasi) akiwaelezea Naibu katibu mkuu pamoja na wafadhili mchakato mzima wa kuipata hati ya hakimiliki ya kimila inavyopatikana.
Mmoja wa watumishi wa LTSP akiwaonesha wageni jinsi kazi ya kupima vipande vya ardhi inavyofanyika uwandani.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kukagua majina yao kama yapo sawasawa kabla ya hati kuchapishwa. Hili ni zoezi muhimu katika kuhakikisha hakuna makosa katika hati itakayochapishwa.

SERIKALI  imedhamilia kuunda mpango mkakati utakaoziwezesha benki nyingi nchini ziweze kutambua hati miliki za kimila ili kuwawezesha  wananchi kujikwamua kiuchumi wakitumia hati zao kama dhamana ya mikopo. Azma hiyo imekuja baada ya kuona mafanikio ya kupima na kurasimisha Ardhi katika Wilaya tatu za mfano za Kilombero,Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro kulikofanywa na wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi kupitia Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi (LTSP).

Akizumgumza baada ya kutembelea Wilaya za Kilombero na Ulanga akiambatana na wafadhili Wa mradi Wa LTSP ili kuona hatua za utekelezaji Wa mradi,Naibu Katibu Mkuu Wa wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mathias Kabundugulu amesema Mradi huo umetekeleza kwa vitendo Sera ya wizara ya miaka mitano. Amesema kwa kipindi cha miaka miwili toka kuanzishwa kwa mradi Wa LTSP mwaka 2016 mafanikio makubwa yameonekana kwa zoezi kwenda kwa haraka zaidi na wananchi wengi kupata hatimiliki za kimila na za vijiji na hiyo ni kutokana na kwenda na teknolojia mpya ya upimaji ya kutumia simu tofauti na teknolojia waliyoanza nayo ikiwemo ya kutumia GPS.

Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kuwa pia amebaini  wananchi katika Wilaya hizo wameupokea vizuri mradi na wameonyesha matumaini na imewapanua kiakili hasa baada ya kuelewa kuwa hati hizo wanaweza kuchukulia mkopo baada ya baadhi ya benki kuanza kuzipokea na kuwapatia mikopo. Hata hivyo Kabundugulu ameonyesha kufurahishwa baada ya kuona akinamama wengi kumiliki hati na kusema kuwa serikali wanajivunia kwani wanaweza kumiliki nguvu ya kiuchumi.

Akizungumzia Mpango Wa wizara kulitunza Bonde LA mto Kilombero,Kabundugulu amesema wizara yake kwa kushirikiana na wizara ya Maliasili na utalii wiki ijayo watatuma timu ya wapimaji na kuweka kambi katika vijiji vyote vyenye muingiliano Wa mipaka na eneo la hifadhi ili kuweka mipaka na kuwaondoa wavamizi wote ili kunusuru eneo hilo ambalo asilimia 65 ya Maji yake yanaingia katika mto Rufiji.

Naye Mkuu Wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya amesema mradi umekuwa na faida kwa wananchi Wa Wilaya yake kwani umemaliza migogoro ya wakulima na wafugaji sambamba na kupunguza migogoro ya mipaka baina ya kijiji na kijiji.

Kwa upande wake Mratibu Wa mradi Wa LTSP Godfrey Machabe amesema toka kuanza kwa mradi wamejaribu kutumia teknolojia tofauti ili kuendana na kasi ya kupima na kuwapatia hati wakazi Wa Wilaya hizo na teknolojia  ya kutumia simu ndio imekuwa na mafaniko makubwa na ana imani ikiendelea kutumika itasaidia kurahisisha upimaji katika maeneo mengi nchini. Machabe ametaja mafanikio ya mfumo Wa kutumia simu kuwa toka waanze kuutumia takribani kwa siku katika wilaya hizo wanazalisha vipande vya Ardhi 1800 tofauti na zamani walipotumia mifumo mingine walikuwa wakizalisha vipande vya Ardhi 400 tu kwa Siku.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad