HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 10 October 2018

MHANDISI WA TANESCO KIZIMBANI KWA TUHUMA YA KUTUMIA MADARAKA YAKE VIBAYA

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
Mhandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Stanslaus Simbila amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la  kutumia madaraka yake vibaya na kupelekea Kampuni ya Zwart  kulipwa kiasi cha EURO 491,622.42 sawa shilingi za kitanzania Bilioni 1,294,260,838.71.

Akisoma hati ya mashtaka dhidi ya mshtakiwa huyo, wakili wa Serikali, Iman Nitume amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wanjah Hamza kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo kati ya June 9 na 19.2010.

Imedaiwa kuwa, siku hiyo mshtakiwa akiwa kama Mhandisi wa Tanesco na Meneja mradi PA/O01/08/HQ/G/123 kati ya Tanesco na Kampuni ya Zwart Technick B.V ambapo kwa nia hovu alitumia vibaya madaraka yake kwa kusaini cheti kilichopelekea kampuni hiyo kupata EURO 491,622.42 sawa shilingi za kitanzania Bilioni 1,294,260,838.71 kabla ya kumaliza kazi waliyopewa.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kufanikiwa kutimiza masharti ya dhamana.

Mahakama imemtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika, watakaotoa fedha taslimu sh. Milioni 100 au kuwasilisha hati ya mali ya isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hivyo cha fedha.

 Kesi imeahirishwa hadi Novemba 8,2018. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad