HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 10 October 2018

KESI YA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TBC KUSIKILIZWA TENA OKTOBA 16 MWAKA HUU

Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Oktoba 16, 2018 itaendelea kusikiliza utetezi wa aliyekuwa Makurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili kwa upande wa mashtaka kumuhoji dhidi ya utetezi alioutoa.

Tido ambaye anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni, alitoa utetezi wake mahakamani hapo Septemba 20, mwaka huu.

Katika utetezi wake, Mhando aliongozwa na mawakili wake, Dk Ramadhani Maleta na Martin Matunda.

Mapema, wakili wa serikali, Emmanuel  Mtumbe aliieleza mahakama kuwa, kesi hiyo Oktoba 9, 2018 ilikuja kwa ajili ya upande wa mashtaka Kuanza kumuhoji Mhando lakini imeshindikana kwa kuwa Wakili, Leonard Swai kutoka Takukuru anayesikiliza kesi hiyo ana udhuru.

 Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma  Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 16 mwaka huu ambapo Tido ataanza kuulizwa maswali na upande wa mashtaka dhidi ya utetezi aliotoa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad