HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 23 October 2018

DKT MAFUMIKO AMEWAASA WADAU WA KEMIKALI KUSIMAMIA USALAMA WA KEMIKALI

MKEMIA Mkuu wa Serikali, Dkt Fidelice Mafumiko leo amewaasa kutunza na kusimamia usalama wa kemikali hatarishi ambazo zinaweza kuleta madhara kwa binadamu.

Ameyasema hayo wakati wa kufungua semina ya wadau wa uhifadhi, udhibiti na usimamizi wa kemikali hatarishi hapa nchini liyofanyika katika ukumbi uliopo BOT jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wadau hao jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa semina hiyo inatawakumbusha na kuwajenge uwezo wadau wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini katika kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2003.

“Nawasihi msikilize kwa makini mafunzo haya ili utakapoanza kwenda kwenye ukaguzi uende kutekeleza matakwa ya Sheria na kanuni zake na sio kwa hiari yako. Kuna vifungu vya sheria ambavyo vinakuhusu kama mkaguzi na utatakiwa kuwajibika pale utakapoenda kinyume chake. Sheria inaainisha wajibu na majukumu ya mkaguzi na pia mkaguliwa, hivyo mnapaswa kuwa makini na kuelewa majukumu na wajibu wenu". amesema Dkt. Mafumiko
Mkemia  Mkuu wa Serikali, Fidelice Mafumiko akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuufungua semina ya mafunzo ya wa wadau mbalimbali wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na udhibiti wa kemikali, Daniel Ndiyo akizungumza wakati wa kuufungua semina ya mafunzo ya wa wadau mbalimbali wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini.


 Baadhi wadau wakiwa katika mafunzo ya wa wadau mbalimbali wa usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini.


Mkemia  Mkuu wa Serikali, Fidelice Mafumiko akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina ya wadau wa uhifadhi usimamizi na udhibiti wa kemikali hapa nchini.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad