HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 23 October 2018

KINDA WA KIKAPU JESCA KUELEKEA SENEGAL KWA MAJARIBIO YA NBA ACADEMY


Nahodha wa timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu chini ya Miaka 18 Jesca Ngisaise anatarajia kusafiri kesho alfajiri  kuelekea Senegal kwenye majaribio


Jesca amekuwa zao zuri la vijana katika mchezo wa kikapu nchini akionekana kufanya vizuri pale anapokuwa anapewa nafasi na kama atafanikiwa kufanya vizuri kwenye majaribio hayo atapata nafasi ya kujiunga na NBA ACADEMY. 

 Kama Jesca atafanikwia kujiunga na NBA Academy atakuwa amepiga hatua moja kubwa sana kuelekea kucheza kwenye WNBA nchini Marekani. 

Jescar mwenye umri wa  miaka 17 na amekua akifanya vizuri katika timu ya Taifa pia aliweza kuchagulia katika timu ya All Stars kwenye mafunzo maalumu ya BWB yaliyofanyika kule Africa kusini mwezi wa nane. Tunamtakia kila la heri aendelee kutuwakilisha vyema. 

Hapa nyumbani Jescar anacheza katika timu ya Ukonga Academy na katika ligi ya mkoa wa Dar es salaam iliyomalizika hivi karibuni alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad